Wekundu wa Msimbazi wahamishia hasira kwa Singida united na kumchakaza

Jumapili ya February 28 Kombe la FA Tanzania liliendelea kwa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa 16 bora dhidi ya klabu ya Singida United katika dimba la Taifa Dar Es Salaam.
Simba ambao waliingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kupata majeraha ya kufungwa na Yanga katika mechi zao mbili za Ligi Kuu, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-1, hivyo Simba wametinga hatua ya 8 bora ya Kombe hilo.
Magoli ya Simba yalifungwa na Danny Lyanga dakika ya 3, Hamis Kiiza dakika ya 18 na 66, na Awadh Juma dakika ya 82 na 86, wakati goli pekee la Singida United lilifungwa na Paul Malamla dakika ya 90 ya mchezo.

Rais Dkt John Pombe Magufuli Awasili Arusha Kuongoza Mkutano Wa 17 Wa Kawaida Wa Wakuu Wa Nchi Wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki

Rais John Pombe Magufuli akiwasili mkoani Arusha tayari kwa mkutano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Mkoani Arusha ambako pamoja na mambo mengine ataongoza Mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Jumatano tarehe 02 Machi, 2016 Mjini Arusha.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Magufuli amelakiwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali pamoja na vikundi vya burudani za ngoma kabla ya kuelekea Arusha Mjini.

Rais Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.Kabla ya kuongoza kikao hicho Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tarehe 03 Machi, 2016 Rais Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya, wataweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha - Holili - Taveta - Voi inayoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.

Barabara hiyo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotekelezwa na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

Walimu Kinondoni kupanda daladala bure

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7FLm-CLAvrtWhJit9qKVsGNWlRK_47S4sPVVTxqKvVUOtwKxw8LCpSoOA35foQpF2vj12PLEkTKnvZf9MdfOw6k8ZNy3p3R-PIri7YJI6P-LySstMC81DIIPXXd3dmo2YhjGzLEaGM2fp/s1600/makonda.jpg
Dc Paul Makonda akitoa ufafanuzi
Mkuu wa wilaya ya Kinondono DC Paul Makonda ameagiza walimu wote wa shule za serikali kupanda daladala bure, ametoa tamko hilo rasm baada ya kikao na madereva pamoja na wamiliki wa vyombo vya usafiri yaani Darcoboa na Uwadar kwakukubaliana kuto wachaji nauri walimu pia Mh Makonda ameeleza msukumo wake mpaka kufikia hatua hiyo kuwa ni
 Moja, kwa kuzingatia changamoto za nauli za mara kwa mara wanazolazimika kuzilipa walimu ili kuyafikia kwa wakati maeneo yao ya kufanyia kazi 
pili, ni kuhakikisha mimi na serikali yangu ya wilaya ya Kinondoni tunakuwa sehemu ya juhudi za Mheshimiwa Raisi za kuboresha maslahi na mazingira ya walimu ya kufanyia kazi ili matarajio ya ndoto yake anayoipigania usiku na mchana ya kutaka kuiona sekta ya elimu nchini ikikua kwa kasi yanatimia. 

Na tatu, ni kuwafanya walimu wa wilaya ya Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla kama watumishi wenzangu wa serikali nao wanafaidi sehemu ya matunda ya serikali yao ambayo kwa dhati imedhamiria kubadilisha maisha yao ili na wao waweze kubadilisha maisha ya vijana wetu kupitia taaluma.

Ngoma Mpya:Smart-Usinune

Ngoma Mpya:Kasu Feat Paick-Skendo Chafu


Jengo la posta Dodoma lateketea kwa moto

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhAQfUr-bINYsp7dmaA6C5YOtvcMaGVUkACEpZeyylFXBGi7ByEV8liEMk8qUSTOWokGBaz6VwDSfhsKfXJMiHxgZTd113ajg7O4o7H-IDrDtqjDSM-GW6v3oMtzZAPOri9WBIIqOUPUdVK/s1600/DFDUO.jpgJENGO Posta lililopo katika eneo la sabasaba katika Manispaa ya Dodoma  jana limeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa
Akizungumzia kutekeleza kwa jengo hilo Meneja wa Posta Mkoa wa Dodoma, Magreth Mlyomi alisema mpaka sasa kuna hasara kubwa kutokana na kutekeleza jengo hilo sambamba na vifaa vyote vya ofisi.
Mlyomi alisema licha ya kuwa hakuna mfanyakazi hata mmoja aliyepoteza maisha katika jengo hilo lakini mpaka sasa kuna vitendea kazi vingi vya ofisi pamoja na mizigo ya wateja imeteketea.

“Kuna mizigo mingi pamoja na vifaa vya kazi vyote vimeteketezwa na moto na kwa taarifa nilizopata kulikuwa na mizigo ya watu, inaonesha kuwa chanzo cha moto ni umeme,” alieleza Meneja huyo.
Akizungumzia kuhusu masuala ya miundombinu ya maeneo husika alisema ni mibovu na kutokana na changamoto hiyo suala hilo lipo katika mamlaka husika ya manispaa.

Kwa upande wake katibu wa wafanyabiashara katika soko la Sabasaba katika Manispaa ya Dodoma, Gergod Lugusi alisema jana saa nne asubuhi kulitokea moto mkali ambao uliunguza jengo hilo.
Alisema chanzo cha moto huo inasemakana kuwa ni tatizo la umeme na uongozi ulilazimika kutoa taarifa katika kikosi cha zima moto na bila kuchelewa walifika kwa wakati.

Hata hivyo alisema licha ya kufika kwa wakati katika tukio bado kikosi hicho kilikutana na kikwazo kwa kutokana na miundombinu kuwa mibovu na migumu kupitika.

Mkurugenzi wa Halmashauri Ya Kondoa Matatani Kwa Upotevu Wa Milioni 180

ASELEMAN Jafo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo

SELEMAN Jafo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, amebaini upotevu wa Sh 180 milioni katika halmashauri ya wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.
Kutokana na kubainika kwa upotevu wa fedha hizo Jafo alitoa saa 48 kwa Hussein Issa ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, kuhakikisha anapeleka maelezo ya kina katika Ofisi ya TAMISEMI juu ya kuibiwa kwa fedha hizo ambazo ni za walipakodi watanzania.
Agizo hilo la Jafo lilitokana ziara ya kikazi iliyofanywa na naibu waziri huyo sambamba na kufanyika kwa kikao cha ndani katika Halmashauri hiyo.

Alisema, Serikali ya Awamu ya Tano haitavumilia kiongozi yoyote ambaye atafanya ubadhilifu kwa fedha ya Umma au jambo lolote ambalo linaonekana kuwepo na alufu ya ufisadi.
Alisema nchi imekuwa ikiendeshwa kimazoea na watu kujilimbikizia mali bila kuwa na hofu ya kuhojiwa jambo ambalo liliwafanya watumishi wa Umma kuwa na kiburi na kufanya kile wanachofikiria.
“Nchi imekuwa ikiendeshwa kimazoea sana watu wanakula hela bila utaratibu na wanafunika funika tu mambo huku wakiwafanya watu kama vipofu, hili haitavumiliwa hata kidogo lazima hatua stahiki zichukuliwe,” alisema.

Jafo alisema, anataka maelezo ya kina juu ya wizi wa fedha hizo na ndani ya masaa hayo 48 anataka awe amepata taarifa pale ofisini kwake.
Sambamba na hilo, aliagiza watu nane wanaotuhumiwa kuhusika na wizi wa fedha hizo wasimamishwe kazi na kukaa pembeni kupisha uchunguzi.
Aidha, aliwaagiza maofisa utumishi na wakuu wa idara kuwajibika na kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.
Naibu wiziri huyo alieleza kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi juu ya watendaji we ngazi ya chini ambao wamekuwa wakionewa na kutopatiwa haki zao kama inavyostahili.

Alisema, watumishi hao wanalalamika kutolipwa malimbikizo yao mbalimbali kama fedha za likizo na kutopandishwa vyeo kwa wakati.

Mh.Kikwete amesema hajahusika kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar kwa kumpigia simu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete amesema hajahusika kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar kwa kumpigia simu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Aliyasema hayo juzi mjini Kibaha wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Chama ya Kibaha Mjini mkoani Pwani na kusema maneno hayo ni ya uongo, hayana ukweli wowote na watu hawapaswi kutoa shutuma hizo juu yake.

Rais huyo wa Awamu ya Nne alisema maneno hayo hayana kichwa wala miguu wala hajawahi kumpigia simu Jecha kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya kufutwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kwani tume hiyo inajitegemea.

“Wasitoe lawama zisizohusika, wapuuzeni sikuwahi kufanya hivyo hata kwa Damian Lubuva wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania hivyo nashangaa watu wanavyosema kuwa nimehusika kufutwa uchaguzi huo,” alisema Kikwete.

“Tume ya Zanzibar ni tume huru na inajitegemea kwani ina mambo yake hata Dk Ali Mohamed Shein (Rais wa Zanzibar) hana uwezo wa kuingilia na kuahirisha uchaguzi huo, watu hao wasipake watu matope wasio husika kwani kila mtu ana nafasi yake,” alifafanua Kikwete.

Alisema kikubwa kinachotakiwa ni kuwaombea Wazanzibari wafanye uchaguzi wao mkuu wa marudio kwa amani na utulivu ili wapate viongozi wao wa kuiongoza Zanzibar na wawaombee wagombea wa CCM washinde.

Aidha, alisema chama hicho kinapaswa kuwaadhibu watu waliokihujumu chama wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kwa kutomwonea mwanachama, bali watende haki na si kwa kwa uonevu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao alisema Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka ameonesha njia ya kiongozi kutumia fursa kuboresha mazingira ya utendaji kazi Awali, Koka ambaye ndiye aliyejenga ofisi hiyo yenye thamani ya Sh milioni 100, alisema aliamua kujitolea kujenga ofisi hiyo kwa lengo la kukisaidia chama kiendeshe shughuli zake.
Koka alisema aliamua kujenga kama kumbukumbu kwa wanaKibaha ili iwe kielelezo cha uongozi wake kama mbunge wa Jimbo hilo kwa ajili ya kufanya shughuli za chama badala ya kufanyia sehemu zisizo na hadhi yao.

Baba Amchoma Mwanawe vidole kisa Mboga Ya Sh. 500

http://1.bp.blogspot.com/-4PZ5K2ZWqeg/VIg46Q4VQZI/AAAAAAAAyg8/Ba4h61KCOFg/s1600/vage.jpgMKAZI wa kitongoji cha Kazima – Kichangani Kata ya Kawajense, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Emmanuel Joseph (31) amemfanyia unyama mtoto wake wa kumzaa, George Emmanuel (4) kwa kuvichoma kwa moto vidole vyake vya mkono wa kushoto, akimtuhumu kukomba mboga yote ya majani aina ya ‘chainizi’ yenye thamani ya Sh 500.
Inasemekana baba huyo amekuwa akiishi na watoto wake watatu baada ya kuachana na mkewe wa ndoa, Semsni Jahala (28) Machi mwaka jana.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Rashid Mohamed amethitibisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema lilitokea juzi saa 12 jioni katika kitongoji cha Kazima– Kichangani.

Akisimulia mkasa huo, Kaimu Kamanda Mohamed alisema mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa mahojiano na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali wa shauri lake kukamilika.
“Jioni hiyo ya tukio saa kumi na moja jioni mtuhumiwa huyo (Emmanuel) alipika chakula cha jioni, ugali na mboga za majani maarufu chainizi kisha akakihifadhi chakula hicho jikoni na kuondoka … aliporudi nyumbani saa kumi na mbili jioni ili kuandaa chakula cha jioni ndipo alipobaini mtoto wake (George) amekomba mboga yote ya majani. 
"Alikasirishwa na kitendo hicho na kusababisha kumpiga kisha kumchoma moto vidole vyake vitatu vya mkono wa kushoto na kumsababishia maumivu makali,” alieleza Kaimu Kamanda.

Kwa mujibu wa mashuhuda kutoka eneo hilo la tukio, mtoto huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambako amelazwa kwa matibabu.
Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda, Oscar Mkenda alisema mke aliamua kuachana na mumewe huyo baada ya kuchoshwa na ukatili na unyanyasaji aliokuwa akifanyiwa, ikiwemo kupigwa mara kwa mara bila sababu yoyote.
“Mtoto George alikomba mboga hizo zote za majani baada ya kushinda na njaa mchana kutwa kwani hata kifungua kinywa hakupa asubuhi… hivyo baada ya baba yake kubaini mtoto wake George amekomba mboga zote, ndipo alipochochea moto na kuukandamiza mkono wake wa kushoto na kuunguza vibaya vidole vyake vitatu,” alieleza Mkenda

Magazeti ya leo haya hapa

Mtoto wa miaka minne jela kwa mauaji huko Misri

Mtoto wa miaka 4 jela maisha kwa mauaji Misri!!Mahakama moja nchini Misri imemUhukumu kifungo cha maisha jela mtoto mmoja wa miaka 4 kwa tuhuma za kufanya mauaji akiwa na umri wa baina ya mwaka mmoja na miwili.
Kwa mujibu wa toleo la mtandaoni la gazeti la New Vision la nchini Uganda, Ahmed Mansour Karmi amepatikana na hatia ya mashtaka manne ya mauaji, manane ya jaribio la mauaji, shitaka moja la wizi wa kutumia mabavu na jingine la kuwatishia maisha askari na maafisa wa polisi wa nchi hiyo, yote hayo akidaiwa kufanya kabla ya kutimiza umri wa miaka miwili. Ahmed ambaye hakuwa kortini wakati wa hukumu hiyo, ni mmoja kati ya watuhumiwa 115 ambao wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa tuhuma za kuhusika na jinai zilizofanywa nchini Misri mapema mwaka 2014. Faisal al-Sayd, wakili wa mtoto huyo amesema kuwa jina la mtoto huyo liliongezwa kwenye orodha ya watuhumiwa kimakosa na kwamba mahakama haikumkabidhi jaji aliyetoa hukumu hiyo, cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo, ili kuhakikisha kuwa alizaliwa Septemba mwaka 2012 au la. Wakili huyo amesema licha ya kukabidhi cheti hicho, lakini mahakama hiyo iliipeleka kesi hiyo katika mahakama ya kijeshi ambapo mtoto huyo alihukumiwa pamoja na watuhumiwa wengine 114. Mwanasheria huyo ambaye alikuwa akizungumza kwa hasira amesema: “Hii inadhihirisha kuwa jaji hakuisoma wala kuitafakari kesi iliyokuwa mbele yake na huu ni ushahidi kwamba hakuna haki nchini Misri.” Ni vyema kuashiria hapa kuwa, zaidi ya wanachama 40,000 wa upinzani wakiwemo wafuasi wa Ikhwanul Muslimin wanazuiliwa katika mazingira ya kutisha katika korokoro za nchini Misri pasina na kufanya kosa lolote. Itakumbukwa kuwa, mwezi Julai mwaka 2013 jeshi la Misri likiongozwa na Jenerali Abdul Fattah al-Sisi lilimpindua Muhammad Morsi, rais wa kwanza kuwahi kuchaguliwa kidemokrasia katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Mafanikio ya Jeshi la Afghanistani dhidi ya Daesh

 
Sambamba na sisitizo la viongozi wa serikali ya Afghanistan katika kukabiliana na magaidi, makamanda wa jeshi wametangaza kusambaratisha ngome kuu ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika wilaya ya Achin mkoani Nangarhar, mashariki mwa nchi hiyo.
Zaman Waziri, mmoja wa makamanda wa jeshi la Afghanistan sanjari na kutangaza habari hiyo, amesema kuwa hivi sasa maeneo mengi ya mkoa huo yako chini ya udhibiti wa askari wa serikali. Fazal Ahmad Shirzad, kamanda wa polisi katika mkoa wa Nangarhar amesema kuwa, katika operesheni dhidi ya magaidi wa kundi la Daesh, askari wa serikali wamewatia hasara kubwa wanachama wa kundi hilo. Aidha kamanda huyo wa polisi amewataka wakazi wa mji wa Achin waliokuwa wamekimbia makazi yao ili kuokoa maisha yao, warejee makwao na kuendelea na maisha yao ya kawaida ingawa pia amewataka washirikiane na maafisa usalama wa seikali dhidi ya magenge ya kigaidi. Kwa mujibu wa viongozi wa eneo hilo, jeshi na askari polisi nchini Afghanistan, wamekuwa wakikabiliana na wanachama wa genge la kigaidi la Daesh kwa kipindi cha miezi minane sasa katika wilaya ya Achin mkoani Nangarhar, mashariki mwa nchi hiyo. Hivi sasa operesheni za kukabiliana na wanachama wa genge hilo, zingali zinaendelea katika kuzisafisha wilaya nne nyingine za mkoa wa Nangarhar nchini humo. Maafisa wa seikali wametangaza pia kwamba katika operesheni za kuusafisha mji wa Achin kutoka mikononi mwa genge hilo, askari wa serikali wamefanikiwa kudhibiti kiasi kikubwa cha silaha na zana za vita zilizokuwa zikitumiwa na magaidi hao. Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh lilikuwa linajaribu kuudhibiti mkoa wa Nangarhar ili kuubadilisha kuwa ngome yao kuu nchini Afghanistan. Hata hivyo njama hizo zimefeli baada ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa jeshi la nchi hiyo. Kwa mujibu wa baadhi ya duru za usalama, jeshi la Afghanistan lilianzisha operesheni kali za kuutwaa mji wa Achin kuanzia tarehe 16 ya mwezi huu wa Februari. Kwa upande wake msemaji wa jeshi la polisi mkoani Nangarhar, Hazrat Hussain Mashriqwal, amesema kuwa katika operesheni hiyo magaidi 50 wa Daesh wameangamizwa. Kwa mujibu wa afisa huyo wa jeshi la polisi, wakazi wa mkoa huo walishirikiana bega kwa bega na askari dhidi ya matakfiri hayo maarufu kwa kutenda jinai dhidi ya binaadamu. Hayo yanajiri katika hali ambayo, katika mwendelezo wa mafanikio ya serikali ya Kabul dhidi ya magaidi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan imetangaza kuwa, imefanikiwa kumtia mbaroni mmoja wa makamanda muhimu wa kundi la kigaidi la Taleban katika mkoa wa Ghor. Gaidi huyo anayeitwa Mawlawi Abdur-Rahman, alinaswa kupitia operesheni maalumu za askari wa polisi katika viunga vya wilaya ya Firuzkuh mkoani Ghor, katikati mwa nchi hiyo. Ripoti za awali zinaeleza kuwa, gaidi huyo alikuwa mratibu wa hujuma za kigaidi katika mkoa huo. Aidha Wizara ya Mambo ya ndani ya Afghanistan imewasisitizia wananchi kuwa jeshi la polisi liko macho na kwamba halitaruhusu maadui kuvuruga usalama wao. Wakati huohuo, wakazi wa miji kadhaa ikiwemo Kabul, mji mkuu wa nchi hiyo sanjari na kufanya maandamano makubwa ya kulaani mashambulizi ya kigaidi, wameitaka serikali kukabiliana vikali na kundi la Taleban na makundi mengine ya kigaidi yanayovuruga usalama wa nchi yao. Washiriki wa maandamano hayo, sanjari na kuunga mkono vikosi vya usalama vya nchi hiyo, wametangaza utayarifu wao kwa ajili ya kukabiliana na magenge hayo ya kigaidi. Ala kulli hal, kusambaratishwa ngome kuu ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika wilaya ya Achin mkoani Nangarhar kunatajwa na weledi wa mambo kuwa hatua moja mbele katika mafanikio dhidi ya makundi ya kigaidi ambayo hivi sasa yanataka kujizatiti katika nchi za Asia ya Kusini na Kati.

Tazama video kali toka kwa Punchline

Video mpya kabisa yenye kiwango cha kimataifa toka kwa msanii anaye julikana kwa jina la Punchline video aliyo ongozwa na muongozaji chipukizi anaye fanya vizuri kwenye tasnia hiyo


Museven Atangazwa Mshindi Wa Kiti Cha Urais Uganda

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi. 
Rais Museveni amepata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu.
Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye amepata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.
Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro nyingi. 
Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.

Chama cha ACT Wazalendo Chamvua Uanachama Ofisa Mipango Na Aliyekuwa Mgombea Urais Zanzibar Kwa Kuhudhuria Vikao Vya ZEC

Chama cha ACT Wazalendo kimemsimamisha uanachama Ofisa Mipango wake, Ali Makame Issa kwa madai ya kukiuka maadili ya chama hicho.
Hata hivyo, Issa alisema jana kuwa hajapokea taarifa yoyote kutoka katika chama hicho.

Hatua hiyo dhidi ya kiongozi huyo mwandamizi ndani ya ACT, imekuja baada ya chama hicho kudai kuwa alishirikiana na aliyekuwa mgombea wa urais wa Zanzibar, Khamis Iddi Lila kuwahujumu.

Awali, Lila alisimamishwa uanachama kwa madai ya kutoa misimamo ya kushiriki uchaguzi wa marudio uliotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha.

Barua ya ACT, iliyosainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Juma Said Sanani imesema: “Kamati maalumu ya Zanzibar imekusimamisha rasmi uanachama kwa mujibu wa katiba ya ACT Ibara ya 11 (2) kuanzia leo Februari 19, 2016, kwa ukiukwaji mkubwa wa katiba Ibara ya 7 (3)(5)(9) Ibara ya 10 (2)(c) (d), Ibara ya 22 (1) (2) (4).”

Barua hiyo inabainisha kuwa mwanachama huyo amekiuka kanuni na maadili pamoja na kukidhalilisha chama.
“Huku ni kukiingiza chama katika mgogoro kwa kuandika barua ya kushiriki uchaguzi wa marudio na kuhudhuria katika kikao cha Tume ya Uchaguzi Februari 17 ukijua kuwa chama kimeshapeleka barua Febuari 9 ya kutoshiriki uchaguzi,” inaeleza.

Vyama vilivyowachukulia hatua viongozi wake kwa madai ya kukiuka kanuni ni Sauti ya Umma (SAU), kilichomfukuza aliyekuwa mgombea wake wa urais wa Zanzibar, Issa Mohamed Zonga, huku Alliance for Democratic Changes (ADC) kikimfukuza aliyekuwa mlezi wake, Hamad Rashid Mohamed

Wata Watatu Watiwa Mbaroni Kwa Kuvamia Kituo Cha Polisi Na Kuvunja Mlango Ili Kuwatoa Wenzao

Kamanda mkuu wa polisi Morogoro Leonard Paul
Watu watatu wamekamatwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuvamia Kituo cha Polisi cha Duthumi na kuvunja mlango kwa lengo la kuwatoa wenzao watatu wanaotuhumiwa kwa wizi wa mifugo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Graifton Mushi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 12.40 jioni.

Alisema polisi walilazimika kutumia silaha za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya watu hao.
Mushi alitaja silaha hizo kuwa ni mapanga, shoka na marungu. Hata hivyo, alisema wakati watu hao wanavamia kituo hicho watuhumiwa hao walishaondolewa kituoni hapo na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati. Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Katika tukio jingine; watu zaidi ya 20 wa Kitongoji cha Mazizini Kijiji cha Maseye Wilaya ya Morogoro wamevamia eneo la mwekezaji Ayubu Mngimbwa na kuteketeza vibanda vilivyokuwa na vifaa mbalimbali vya uchimbaji wa madini na kumshambulia kwa vipigo.
Kaimu Kamanda huyo alisema thamani ya vibanda na vifaa vilivyoteketezwa bado haijafahamika.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro kati ya wananchi wa kitongoji hicho na mwekezaji anayedaiwa kutiririsha maji yenye kemikali za sumu

Breaking News: Matokeo Ya Mtihani Kidato Cha Nne -2015 Yametoka....Yatazame Hapa

Waziri wa elimu dk Shukuru Kawambwa
Baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.
  Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.
Msonde amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
 
Amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.
Aidha kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.
Kwa upade wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, Msonde amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.
 
Aidha waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.
Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wasichana 38,338 sawa na asilimia 19.63.
Amesema kwa upande wa ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule, ufaulu wa juu kabisa ni wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 wamefaulu huku ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 16.76 wamefaulu.
 
Matokeo hayo yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya ule wa wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi hivi karibuni.

Yanga yaibuka kidedea tena

Hiki ndio kikosi cha Yanga kilicho peleka msiba Msimbazi ambapo Yanga ilishinda kwa mabao 2_0 huku mabao hayo yakiwekwa kimyani na Tambwe na Ngoma katika uwanja wa Taifa jiji Dar es salaam wakati huo huku Yanga wakiwa na historia ya mwaka jana kwenye mechi kama hii Simba waliibuka kidedea kwa ushindi kama walio upata Yanga leo

Madiwani waendelea kubana wachafuzi mazingira

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro limeendelea kusimamia uboreshaji mazingira kwa kuwatoza faini wafanyabiashara wasiofuata utaratibu wa usafi kwa kuwafikisha mahakamani.
Hatua hiyo inatokana na kuwepo ugonjwa wa kipindupindu tangu Augosti mwaka jana, ambapo hadi Februari 14, mwaka huu watu 10 walipoteza maisha.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga alisema hayo juzi, wakati akiwasilisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2016/2017 katika kikao cha bajeti cha baraza hilo.
Alisema, halmashauri hiyo ilipata kipindupindu Agosti hadi Oktoba mwaka jana, ambapo wagonjwa 117 walitambuliwa na wengine wawili walipoteza maisha hadi ulipodhibitiwa.
“Mlipuko wa kwanza ulidhibitiwa kwa kufanya usafi, kutoa elimu ya afya na kuhamasisha matumizi ya dawa za kutakasa maji,” alisema Meya huyo.
Pamoja na juhudi hizo, alisema ugonjwa huo ulianza tena Desemba 23 mwaka 2015 kwa mara ya pili, wakati wa sikukuu za Idd na Krismasi na kusababisha idadi ya wagonjwa na vifo kuongezeka.

Ulinzi kwa Watanzania walioko India kuimarishwa yasema serikali ya India

Balozi Ramadhani Mwinyi akitoa maelezo
SERIKALI imesema itaendelea kuhakikisha wanafunzi wanaosoma nje wanakuwa katika mazingira salama, na tayari watu watano waliohusika na tukio la kushambuliwa kwa wanafunzi wanne wanaosoma India wanashikiliwa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Ramadhan Mwinyi aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akitoa ufafanuzi wa tukio lililotokea Bangalore India.
“Tulipata taarifa kuwa wananchi wetu ambao ni wanafunzi wa Bangalore India walishambuliwa baada ya raia wa Sudan kumgonga raia wa India kwa gari na kisha kufariki dunia, ambapo kuanzia hapo palitokea mtafaruku wa kushambulia watu wenye asili ya Afrika waliokuwepo maeneo hayo,” alieleza Balozi Mwinyi.
Alisema baada ya tukio hilo wanafunzi hao wa Kitanzania wakitokea chuo walisimama maeneo hayo ili kujionea ni nini kimetokea lakini wao pia walichanganywa na kuanza kushambuliwa na raia hao wa India kwa kuwa walikuwa hawatofautishi watu, bali walikuwa wakishambulia raia wote wenye asili ya Kiafrika.
“Katika tukio hilo raia wetu wanne walishambuliwa vibaya na baadaye walipelekwa hospitali na kupatiwa matibabu. Kufuatia hilo balozi wetu nchini humo amefuatilia hili na ameandika barua ya kibalozi kutaka Serikali ya India kueleza ni kitu gani kimetokea na kueleza jinsi gani wanawalinda raia wetu,” alieleza.
Aidha, alisema jana Balozi wa Tanzania nchini humo amefanya ziara ya kutembelea jimbo hilo na atazungumza na raia ili kuhakikisha usalama wao unalindwa.
Pia alisema jana alimuita Balozi wa India nchini na kufanya naye mazungumzo na alimhakikisha kwamba tayari hatua zimeshachukuliwa na tamko limeshatolewa la kilichotokea Bangalore na wameahidi kwamba watahakikisha wahusika wote wanakamatwa na kuchukuliwa hatua.
Alisema katika hatua za awali tayari watu watano wameshakamatwa na ulinzi wa wanafunzi umeimarishwa na kuahidi wataimarisha usalama zaidi ili wananchi walio nje waishi kwa usalama na mabaya zaidi yasijitokeze.
Aidha, Balozi Mwinyi alisema kuna tukio lingine limetokea juzi jioni la mwanafunzi Mtanzania Christian Benjamin Mutandisi aliyekuwa akisoma Chuo cha Koshys ambaye alipata ajali ya pikipiki na kufariki dunia papo hapo na kubainisha kwamba baada ya uchunguzi wamegundua kwamba ajali hiyo haihusiani na tukio la Bangalore

Serikali yajieleza bungeni kukatika kwa umeme

SERIKALI imesema tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini linatokana na uchakavu na kuzidiwa kwa vituo vya kupoza umeme na miundombinu ya usafirishaji na usambazaji nishati hiyo.
Katika kukabiliana na tatizo hilo Tanesco inachukua hatua za kujenga mifumo ya njia kubwa za umeme wa msongo wa kilovoti 400 (Iringa- Dodoma-Singida-Shinyanga), gridi ya Kaskazini Mashariki (Dar es Salaam, Chalinze,Tanga –Arusha), ya Kaskazini Magharibi (Geita- Kagera –Katavi- Kigoma- Rukwa na Mbeya) na Makambako- Songea wa kilovoti 220.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani wakati akijibu swali la Mbunge wa Magu, Boniventure Kiswaga (CCM). Kiswaga alitaka kufahamu serikali imejipangaje kukabiliana na tatizo la kukatika katika kwa umeme.
Pia mbunge huyo alitaka kufahamu, Je serikali itakamilisha lini kupeleka umeme katika vijiji vya jimbo hilo ikizingatiwa mpaka sasa ni asilimia 20 tu ya vijiji ndiyo vina umeme. Kalemani akijibu swali hilo, alisema tatizo la kukatika kwa umeme linatokana na uchakavu na kuzidiwa kwa miundombinu ya kupoza umeme pamoja na matukio ya kulipuka kwa transfoma yanayosababishwa na radi hasa kipindi cha mvua pamoja na wizi wa mafuta ya transfoma unaofanywa na wananchi wasio waaminifu.
Alisema Tanesco inakamilisha upanuzi wa usambazaji wa umeme katika majiji makubwa ya Arusha, Dar es Salaam, na Mwanza ambapo kazi hizo zitahusisha ujenzi wa njia mpya za umeme na kupanua vituo vya kupoza umeme.
“Kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro kumeimarisha upatikanaji wa umeme maeneo ya Mirerani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA),” alisema Kalemani.
Pia vituo vya kupoza umeme katika jiji la Dar es Salaam vya Gongo la Mboto, Kipawa, Mbagala, na Kurasini vitaunganishwa kwa njia ya sakiti mzunguko kutoka Ubungo na Kinyerezi kuanzia Machi mwaka huu.

RC acharukia waliofelisha watoto la 7 Tabora

Mkuu wa mkoa wa Tabora mh.Ludovick Mwananzila
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Ludovick Mwananzila (pichani), amewaagiza wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya kuwaandikia barua za onyo walimu wakuu wote wa shule za msingi waliofaulisha watoto chini ya 10 huku akiwataka pia kuwaondoa mara moja katika madarasa husika walimu waliofaulisha watoto chini ya saba.
Alitoa maagizo hayo jana katika mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika Ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi, mjini hapa. Alisema walimu hao wameshindwa kufaulisha kutokana na uzembe na wameshindwa kufanya kazi waliyotumwa na serikali, na kwamba walimu wakuu wameshindwa kuwasimamia wa chini yao ili wafundishe hivyo ambao hawakufundisha ipasavyo na ndio maana yametokea matokeo mabaya ya ufaulu wa darasa la saba 2015.
Aidha, alisema uzembe na vitendo vya ulevi kwa baadhi ya walimu vimechangia pia kufanya vibaya kwa watoto, kwani muda mwingi wanautumia kwenye mambo yao binafsi ikiwemo biashara za bodaboda, ulevi na nyinginezo na sio kufundisha watoto darasani.
Akionesha kuchukizwa na ufaulu duni, Mwananzila aliwaagiza wakurugenzi watendaji wa Halmashauri zote kuwasilisha kwake majina ya walimu walevi na wanaojihusisha na biashara mbalimbali, akisema vitu hivyo vinachangia kurudisha nyuma maendeleo ya elimu. Aliwataka wakuu wa wilaya kusimamia maagizo hayo na kuhakikisha taarifa hizo zinamfikia haraka ili achukue hatua stahiki kwa wahusika.

Chama kipya cha siasa chapata usajili wa muda

Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi
MSAJILI wa Vyama vya Siasa Tanzania, Jaji Francis Mutungi jana alikabidhi cheti cha usajili wa muda kwa chama kipya cha siasa cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA).
CM-TANZANIA ni chama cha 23 kupokea usajili baada ya vyama vingine vya siasa 22 vyenye usajili wa kudumu.
Akikabidhi cheti hicho Dar es Salaam jana, Jaji Mutungi aliviasa vyama vya siasa nchini kuepukana na migogoro na kutumia vikao vyao katika kuendeleza shughuli zao za kisiasa.
Aidha, Jaji Mutungi amevitaka vyama vya siasa nchini kufanya siasa na sio uanaharakati kwani kwa kufanya hivyo malengo yao yatatimia na kuifanya Tanzania kuwa na amani.
“Msipende kukimbilia kwenye vyombo vya habari mnapokuwa na migogoro, bali malizeni tofauti zenu ndani ya vikao vyenu kulingana na Katiba ya vyama vyenu,” alisema Jaji Mutungi.
Aliongeza kuwa Tanzania inapaswa kuwa na vyama vya siasa vinavyojitambua na vinavyojua wajibu wao katika kuleta maendeleo ya Taifa kwani siasa sio chuki wala uhasama.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA), Laban Nkembo alisema chama hicho kimeanzishwa kwa lengo la kuiweka Tanzania kimaadili na uwajibikaji kwa kuwa kinabeba mambo makubwa mawili yakiwemo amani na upendo.
Aliongeza kuwa chama chao sio cha upinzani na kinaheshimu chama kilichopo madarakani hivyo, kinaahidi kushirikiana na chama tawala kuenzi mazuri yanayofanywa na chama hicho.

Mkoa mpya wa Songwe na wilaya mpya zaainishwa

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ameidhinisha kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Songwe na wilaya nyingine mpya nchini

Akitoa tamko hilo kwa niaba ya Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simbachawene amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa Mamlaka Rais ya kugawa Nchi kwa kadri ambavyo atakapoona inafaa.
Mhe George Simachawene amesema kutokana na mamlaka hayo aliyopewa Rais jumla ya Wilaya sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa Songwe umeanzishwa kutoka Mkoa wa Mbeya.

Amezitaja Wilaya mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe,Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi

“ Nichukue fursa hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Wilaya mpya zimeanzishwa kufanya maandalizi rasmi ili Mkoa na Wilaya hizo ziweze kuanza kufanya kazi,aidha mkazo uwekwe kwenye upatikanaji wa Ofisi na huduma zote muhimu kupatikana kwa urahisi katika Mkoa naWilaya hizo mpya” Alisema Mhe Simbachawene.

LHRC Wamtaka Mwenyekiti wa ZEC Kujiuzulu Mara Moja......Chama cha CCK Chamvua Uanachama Katibu Wake Aliyetangaza Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar

 
Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimemtaka Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salum Jecha ajiuzulu wadhifa huo kutokana na hatua aliyochukuwa ya kufuta uchaguzi na kutangaza tarehe ya kurudiwa bila kufuata sheria hivyo kumemuondolea sifa ya kusimamia na kuongoza tume hiyo.

Tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Bi Imelda Urrio ambapo amesema ukosefu wa taarifa sahihi na rasimi za michakato ya maridhiano toka kufutwa kwa uchaguzi kunaondoa imani ya wananchi juu ya viongozi wao, tume na mchakato mzima wa chaguzi za kidemokrasia Zanzibar.

Amesema kuwa kufutwa na kutangazwa upya kwa uchaguzi wa Zanzibar kunakiuka katiba,sheria,na kanuni za uchaguzi na pia misingi ya demokrasia ya utawala wa  sheria nchini.

Amesema kuwa katiba ya Zanzibar na sheria za uchaguzi hazijampa mamlaka mwenyekiti na hata tume yote kufuta uchaguzi na hivyo kilichotokea Zanzibar kimeaacha watanzania wakiwa hawaelewi ni sheria na katiba ipi imetumika kufuta uchaguzi huo.

Bi Imelda ameongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 123 cha sheria ya uchaguzi Zanzibar mtu akishachaguliwa uchaguzi wake hautohojiwa isipokuwa kwa kupeleka shauri mahakamani,hivyo kwa msingi huo LHRC wanaona kwamba hakuna kifungu chochote cha sheria kinachoipa tume ya uchaguzi au mwenyekiti wake mamlaka ya kufuta uchaguzi na kuamuru marudio isipokuwa kwa amri ya mahakama.

Wakati huohuo chama cha kijamii CCK kimemsimamisha kazi na uanachama naibu katibu mkuu wake wa Zanzibar Ali Khatib Ali ambaye pia alikuwa mgombea urais wa Zanzibar kwenye uchaguzi uliotangazwa kufutwa na ZEC Oktoba 2015.

Mwenyekiti wa CCK Costantine Achitanda amesema chama kimefikia maamuzi hayo ili kupisha uchunguzi dhidi yake kufuatia uamuzi wake binafsi wa kutangazia umma kuwa CCK itashiriki uchaguzi wa marudio huko Zanzibar kinyume na taratibu za chama.

Wakili Hamis Mkindi kutoka LHRC akiongea.Kushoto  ni  kaimu mkutugenzi wa kituo cha sheria na Haki za binadamu Bi Imelda Lulu Urio

 Waandishi  wa  habari  wakifuatilia  habari hiyo

Binti wa Kitanzania Anayesoma India Adhalilishwa Kwa Kupigwa Na Kuvuliwa Nguo


Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 21 (jina linahifadhiwa) anayesoma shahada ya biashara, mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Acharya, Bangalore, alifanyiwa ukatili huo akiwa na Watanzania wengine wanne.
Gazeti la Deccan Chronical la Bangalore, liliripoti kuwa tukio hilo lilitokea Januari 31, baada ya mwanafunzi raia wa Sudan, Ismail Mohammed kugonga gari la raia mmoja wa India, mkazi wa Hesaraghatta aliyekuwa na mkewe na kusababisha kifo cha mama huyo.

Nusu saa baadaye, Watanzania watano akiwamo aliyevuliwa nguo, walifika katika eneo hilo wakiwa kwenye gari ndipo kundi la watu hao lilipoanza kumshambulia binti huyo, kisha kumvua nguo na kumlazimisha atembee uchi.
Baada ya kuchoma gari lililosababisha ajali hiyo, kundi hilo pia liliteketeza gari alilokuwamo Mtanzania huyo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mindi Kasiga alisema Balozi wa Tanzania nchini humo, John Kijazi ameshakutana na wanafunzi hao na ameshazungumza na Serikali ya India kuhusu tukio hilo.

Gazeti la Deccan Chronical liliripoti kuwa licha ya polisi waliokuwapo eneo hilo hawakuchukua hatua yoyote hata pale msamaria mwema aliyejitokeza kumsitiri msichana huyo kwa fulana yake ambaye pia alipigwa huku fulana hiyo ikichanwa.
Mshauri wa masuala ya sheria kwa wanafunzi kutoka Afrika wanaosoma Bangalore, Bosco Kaweesi alinukuliwa na gazeti la The Chronical akisema hata dereva wa gari alilokuwa  Mtanzania huyo, Micah Pundugu alipigwa na kujeruhiwa vibaya.
 Alisema hata pale msichana huyo alipojaribu kupanda basi ili kujinusuru na zahama hiyo, abiria walimshusha.

Wabunge Wa CCM Wamgomea Magufuli


Kikao cha siri cha wabunge wa CCM kilichoitishwa juzi usiku kujadili mipango ya Serikali kudhibiti matumizi, kimefanikiwa kukwamisha uamuzi wa kuzitaka halmashauri na mashirika ya umma kuingiza mapato yake yote kwenye mfuko mkuu.

Mpango huo, ambao pia ulipingwa na wabunge kutoka vyama vya upinzani, ulilenga kuondoa utaratibu uliopo wa halmashauri, mashirika na taasisi za Serikali kukusanya mapato yake na kuzitumia na badala yake zilitakiwa ziingize mapato hayo kwenye mfuko mkuu na baadaye Serikali itoe fedha kulingana na bajeti inazopelekewa.
Juzi, katika mjadala wa mwongozo wa Mpango wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2016/17, wabunge hao walipinga uamuzi huo wakisema utaziua halmashauri na wakataka mashirika ambayo yanamilikiwa na Serikali ndiyo yapeleke fedha kwenye mfuko huo. 
Kutokana na mvutano huo, juzi usiku wabunge wa CCM walikutana katika kikao cha ndani kilichofanyika makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma, kujadili jambo hilo na kushauri libadilishwe ili kuziokoa halmashauri nchini.

Jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alisema  kuwa tayari Serikali imetoa maelezo.
“Tumetoa maelezo kuwa hatukumaanisha halmashauri wala mifuko ya hifadhi za jamii. Suala hili litayahusu mashirika ya umma pekee,” alisema Simbachawene.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa wabunge hao walimbana Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kwamba uamuzi huo utazifanya halmashauri kukosa fedha za kufanya miradi yake mbalimbali ikwame.

“Mkutano ulianza saa mbili usiku na kumalizika saa tano usiku. Tulichokubaliana na kufanyika kwa marekebisho ili halmashauri ziendelee na utaratibu kama wa awali, pia kuitaka Serikali kutoihusisha mifuko ya hifadhi za jamii katika suala hili,” alisema mbunge ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.

“Fedha zitakazokwenda katika mfuko huo ni za mashirika kama Tanesco na Tanapa.Lengo hapo ni kuweka utaratibu mzuri wa matumizi kwamba shirika linaingiza fedha zake katika mfuko, likihitaji fedha litapelekewa kulingana na utaratibu utakaowekwa.”

Chanzo hicho  kilieleza kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii haitaguswa kwa sababu fedha zake ni za wanachama na hutumika kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali.

“Wabunge pia walihoji kama fedha hizo zitaweza kutoka katika mfuko huo na kuzifikia halmashauri katika kipindi hiki ambacho fedha nyingi zinashindwa kufika kwa wakati kutekeleza miradi ya maendeleo,” alisema mbunge mwingine.
Jana, katika mjadala wa mpango huo hakuna mbunge wa CCM wala wa Ukawa aliyegusia suala hilo, kitendo kinachotafsiriwa kuwa jambo hilo limeondolewa kabisa. 
Wachangia mjadala 
Akichangia mjadala wa mpango huo, Mbunge wa Lulindi (CCM), Jerome Bwanausi aliishauri Serikali kuachana na vyanzo vya mapato vilivyozoeleka, badala yake itafute vyanzo vipya.

Katika mpango huo, Serikali ilitaja baadhi ya vyanzo vyake vya ndani vya mapato kuwa ni kodi katika vinywaji mbalimbali, sigara, muda wa matumizi wa simu za mkononi na kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). 
Katika eneo hilo imeweka uwekezako wa kukusanya Sh4 trilioni. “Watendaji wa Serikali lazima wajifunze kutoka katika taasisi ambazo zina vyanzo vingi vya mapato. Mapato yako mengi tu hata katika nyumba za kupanga na kuziwezesha halmashauri kukusanya mapato zaidi,” alisema.
Mbunge wa Hanang’(CCM), Dk Mary Nagu alisema uchumi wa viwanda unategemea kilimo, mifugo na uvuvi na kuitaka Serikali kuhakikisha inatilia mkazo sekta hizo kwa maelezo kuwa itasaidia kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Anatropia Teonist alionyesha wasiwasi juu ya utekelezaji wa mipango huo wa Serikali, kutokana na mawaziri wengi kufanya kazi kwa kutafuta sifa katika vyombo vya habari.
Alimtaja Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kwamba anahusika katika uporaji wa viwanja vya wananchi. 
“Katika sekta ya ardhi kuna matatizo makubwa. Migogoro ya ardhi inarudisha nyuma maendeleo ya watu kwa kiasi kikubwa. Pale Dar es Salaam sasa mnavunja nyumba za watu wa mabondeni. Kutokana na zoezi hilo, zaidi ya watu 99, 000 watakuwa hawana makazi,” alisema.

Alisema kasi ya Serikali kuwaletea wananchi maendeleo ni ndogo na kwamba kwa kipindi cha miaka 15, Serikali imepunguza umasikini kwa asilimia 14 tu.


Magazeti ya leo tarehe 4Februari 2016


©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved