Madiwani waendelea kubana wachafuzi mazingira

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro limeendelea kusimamia uboreshaji mazingira kwa kuwatoza faini wafanyabiashara wasiofuata utaratibu wa usafi kwa kuwafikisha mahakamani.
Hatua hiyo inatokana na kuwepo ugonjwa wa kipindupindu tangu Augosti mwaka jana, ambapo hadi Februari 14, mwaka huu watu 10 walipoteza maisha.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga alisema hayo juzi, wakati akiwasilisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2016/2017 katika kikao cha bajeti cha baraza hilo.
Alisema, halmashauri hiyo ilipata kipindupindu Agosti hadi Oktoba mwaka jana, ambapo wagonjwa 117 walitambuliwa na wengine wawili walipoteza maisha hadi ulipodhibitiwa.
“Mlipuko wa kwanza ulidhibitiwa kwa kufanya usafi, kutoa elimu ya afya na kuhamasisha matumizi ya dawa za kutakasa maji,” alisema Meya huyo.
Pamoja na juhudi hizo, alisema ugonjwa huo ulianza tena Desemba 23 mwaka 2015 kwa mara ya pili, wakati wa sikukuu za Idd na Krismasi na kusababisha idadi ya wagonjwa na vifo kuongezeka.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved