Mabomu yalipuka Zanzibar

MABOMU mawili yanayosadikiwa kuwa yalitegwa na watu wasiojulikana, yamelipuka yenyewe na kuzua taharuki kubwa katika eneo la Michenzani mjini hapa. Kamanda wa Kikosi cha Operesheni na Mafunzo cha Jeshi la Polisi Zanzibar, Juma Yussuf alithibitisha jana kulipuka kwa mabomu hayo.
Alisema uchunguzi zaidi un aendelea, kujua wahusika wa matukio hayo. Juzi askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), walifanikiwa kutegua bomu moja, lililotengwa karibu na Kituo cha Polisi cha Darajani bila ya kusababisha madhara.
Matukio hayo, mawili yamezua hofu na wasiwasi kuhusu amani na usalama wa wananchi wa Zanzibar. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haijatoa tamko kuhusu matukio hayo pamoja na mustakabali wa hali ya kisiasa ya Zanzibar, baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi mkuu wa Oktoba 25.
Tamko la CCM
Wakati huo huo, Chama Cha Mapindizi (CCM) Zanzibar kimetoa tamko na kuunga mkono uamuzi wa ZEC kufuta Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu kutokana na ukiukwaji kwa taratibu za kisheria.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akizungumza na waandishi wa habari Ofisi Kuu Kisiwandui mjini hapa, alisema jana kuwa uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, ulikuwa na dosari nyingi, ambazo zilitosha kuufanya kuwa si huru na haki.
Alisema kitendo kilichofanywa na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kutangaza matokeo ni ukiukwaji wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Ibara ya 11 Kifungu 42 (5) na lengo lake ni kuanzisha mgogoro wa kisiasa na vurugu.
“Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kinatoa tamko na kutaka uchaguzi mkuu urudiwe kwa sababu ulijaa kasoro nyingi, kiasi ya kuufanya si tena uchaguzi isipokuwa na uchafuzi,” alisema.
Kwa mfano, Vuai alisema mawakala wa CCM walinyimwa shahada za kuwepo katika vituo vya kupigia kura, kitendo kilichodhihirisha kulikuwa na lengo la kuvuruga na kupendelea chama kimoja ili kishinde uchaguzi huo.
Pia, alisema CCM inaishutumu ZEC, ikiwemo makamishna wake, kwamba wanapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kusimamia uchaguzi huo vizuri na kujaribu kuingiza nchi katika machafuko. Vuai aliwataka wanachama wa CCM kuwa watulivu na kuacha kuruhusu vijana wao, kujiingiza katika vurugu, ambazo zimeitishwa na CUF.
Alisema matamshi yaliyotolewa na Maalim Seif, kwamba ataruhusu vijana kuingia barabarani ni ya uchochezi, ambayo yanatakiwa kuchukuliwa hatua na vyombo vya dola. Tangazo la ZEC Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha, wiki hii alitoa “Taarifa Kwa Umma ya Kufuta Uchaguzi wa Zanzibar”.
Katika taarifa hiyo, Jecha Salim Jecha alisema “Mimi nikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, nimeridhika kwamba uchaguzi huu haukuwa wa haki na kuna ukiukwaji mkubwa wa Sheria na taratibu za uchaguzi. Hivyo, kwa uwezo nilionao natangaza rasmi kwamba uchaguzi huu na matokeo yake yote yamefutwa na kwamba kuna haja ya kurudia uchaguzi huu”

CHELSEA WAPIGWA NA LIVERPOOL BAO 3-1

1
Wachezaji wa timu ya Liverpool wakimpongeza Philippe Coutinho (katikati) baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika  45 kipindi cha kwanza katika Uwanja wa Stamford Bridge.

Timu ya Chelsea leo imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Stamford Bridge baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Liverpool.
Chelsea inayonolewa na Kocha Mreno, Jose Mourinho ilishindwa kulinda bao lake la mapema ililolipata dakika ya nne kupitia kwa kiungo Ramires.
Hii inakuwa mechi ya kwanza kwa Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp kupata ushindi kwenye EPL tangu ajiunge na kikosi hicho mapema mwezi huu.
Aidha inaweza kuwa mechi ya mwisho kwa Mourinho kuendelea kukinoa kikosi cha Chelsea kwani alipewa mechi mbili kuhakikisha anashinda ikiwemo hii ya leo lakini zote amepoteza.
Chelsea (4-2-3-1): Begovic 6; Zouma 5, Cahill 6, Terry 6, Azpilicueta 6 (Falcao 75, 6); Ramires 7, Mikel 6.5 (Fabregas 69, 6), Willian 7; Oscar 6.5, Hazard 5 (Kenedy 59, 6), Costa 6
Subs not used: Baba, Remy, Matic, Amelia
Scorer: Ramires 4
Booked: Mikel
Liverpool (4-3-3): Mignolet 6; Clyne 7, Skrtel 7, Sakho 7.5, Moreno 5.5; Can 6.5, Lucas 6.5, Milner 7 (Benteke 64, 7); Lallana 7.5 (Lovren 90), Coutinho 8.5, Firmino 7.5 (Ibe 75, 6.5)
Subs not used: Allen, Bogdan, Teixeira, Randall
Scorers: Coutinho 45+3, 74, Benteke 83
Booked: Coutinho, Lucas, Can, Benteke
Att: 41,577
Referee: Mark Clattenburg

WATU SITA WAFA AJALINI MIKUMI MKOANI MOROGORO

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Leonard Paul.
Watu sita wamepoteza maisha baada ya gari waliyokuwa wanasafiria kugongana uso kwa uso na basi linalomilikiwa na kampuni ya Prince Muro.
Ajali hiyo imetokea leo eneo la Mikumi majira ya saa sita kasorobo baada ya gari aina ya Noah  lililokuwa linatoka mikumi kwenda Morogoro Mjini kupasuka tairi la mbele (kulia), kupoteza mwelekeo na kisha kugongana na basi la Prince Muro lililokuwa linatoka Dar es Salaam kuelekea Tunduma mkoani Mbeya.
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Leonard Paul amewaambia waandishi wa habari mjini humo kuwa katika ajali hiyo watu wote sita waliokuwa wanasafiri kwa Noah hiyo walifariki dunia papo hapo huku baadhi ya abiria wa basi la Prince Muro wakipata majeraha madogo.
Kamanda Paul amesema kati ya marehemu sita wa ajali hiyo, wanne ni wanaume na wawili ni wanawake.
Alisema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro ikisubiri utambuzi na kwamba majeruhi wametibiwa katika hospitali ya Mtakatifu Kizito iliyopo mjini Mikumi na kuruhusiwa kuendelea na safari.
Amesema baada ya ajali kutokea jeshi lake lilifanya upekuzi kwenye Noah na kufanikiwa kupata vitambulisho vinne na kusema vitasaidia katika mchakato wa kuwatambua marehemu.
Akizungumzia chanzo cha ajali hiyo, Kamanda Paul amesema mashuhuda wa ajali hiyo wamesema dereva wa Noah alikuwa kwenye mwendo kasi hivyo kushindwa kulimudu gari mara baada ya tairi kupasuka.
©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved