Je umeisikiliza moja ya Soundtrack za Ganga Njaa?

Ikiwa ni moja ya filamu zinazotegemewa kutoka hivi karibuni ndani ya mkoa wa Mbeya,Ganga Njaa imezidi kupasua milango kwa kutengeneza nyimbo maalum kwa ajili ya filamu hiyo.Wimbo huu ukiwa umetengenezwa na 'producer' Necka Beat kutoka T-Motion Music umeimbwa na msanii na mwandishi mahiri wa nyimbo anayefahamika kwa jina la Meshamazing.Huu ni bonge la wimbo,sikiliza upate maudhui ya filamu ya Ganga Njaa (Japo kidogo).Filamu hii imefanywa na kampuni ya Greenwood Living Pictures.
'Download' wimbo hapa

Fide Losso,Goliath na Lastie Bone Kuungana?

Je hili ni kundi?Wako chini ya menejimenti yoyote?

Vipi kuhusu T-Block na Makanta?Goliath kutorudi Mwanza?

Fidelosso naye kajitoa MCB?

Hapa juzi kati,timu ya New Day Taarifa ilifika katika moja ya Studio kubwa ndani ya Mbeya iitwayo Makanta Records ndipo ilipofanikiwa kukutana na wasanii machachari watatu huku wakiwa wanajiita FLG.
Wasanii hao ni Fidelosso,Lastie bone na Goliath.Baada ya hapo NDT ikawauliza nia ya wao kujuinga na kuunda FLG na nini maana yake?,Goliath akajibu akisema "FLG ni kifupisho cha majina yetu wote watatu","Kwanza FLG siyo kundi,ila ni muunganiko wa muda mfupi kwa ajili ya 'project' tunayoifanya kwa sasa"alijibu Lastie Bone"Pia hatuna menejementi yoyote ni sisi wenyewe tumeamua kusimama na kufanya kitu hichi"aliongeza.
"Kwa upande wangu mimi bado niko MCB,na wala haiingiliani na FLG"Alijibu Fidelosso.
Lilipokuja swala la Goliath kuwepo Mbeya au kurudi Mwanza,yeye mwenyewe akadai kuwa bado yupo Mbeya kwani hajamaliza masomo yake ya chuo,hivyo ana muda mwingi wa kumuwezesha kufanya 'projects' nyingi zaidi.
"T-Block na Makanta bado ni viwanja vyangu vya nyumbani,hii 'project' ni binafsi tu na haimaanishi nimeamua kujitegemea" Aliongeza Lastie Bone.
FLG walielezea kuwa wameazimia kufanya  'project' hii ili iwafikishe hatua mpya katika muziki,na kwa sasa tayari wamekwisha fanya nyimbo nne,na zimebaki nne tu ili kukamilisha Albamu yao ambayo bado hawajaipa jina.

Wasanii wa Chunya waungana na Kutoa wimbo

Lastie Bone kahusika pia 

Kati yao yupo dogo wa miaka 17

Wasafiri hadi Mbeya Mjini kutafuta Studio

Kenny Eyes,moja ya wasanii mahili wa Chunya

 

Kutokana na kukua kwa tasnia ya muziki wa kizazi kipya ndani ya mkoa wa Mbeya na Nyanda za juu kusini,ushirikiano katika kuwasilisha ladha tofauti unaonekana kuleta chachu.
Jambo hilo limewafanya vijana kadhaa wanowakilisha wilaya ya Chunya kujikusanya na kutoa wimbo wa pamoja."Ilitubidi tusafiri hadi Mbeya mjini ili kufanya wimbo wenye kiwango kizuri"Aliongea Kasu,mmoja ya wasanii hao."Binafsi namkubali sana Lastie Bone na ndiyo maana nikakubaliana na swala la kumuweka yeye kuwa 'producer' wa wimbo,na kweli hakautendea haki"aliongezea Kenny Eyes.
Ndani ya wimbo huu,wasanii hawa wameelezea swala la watu kuleta dharau kutokana na kumchukulia mtu kutokana na wanavyomuona.Wimbo huuu umeitwa "Usilete Madharau".
"Kabla ya jina hili,tuliuita 'Kabla hujania',lakini kutokana na ujumbe mkubwa uliopo ndani yake,nikapendekeza uitwe 'usilete madharau' na wasanii wakakubaliana nam"Aliongea Lastie Bone,'producer' wa wimbo huo.

Sikiliza na kuupakua wimbo huo HAPA
©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved