Fide Losso,Goliath na Lastie Bone Kuungana?

Je hili ni kundi?Wako chini ya menejimenti yoyote?

Vipi kuhusu T-Block na Makanta?Goliath kutorudi Mwanza?

Fidelosso naye kajitoa MCB?

Hapa juzi kati,timu ya New Day Taarifa ilifika katika moja ya Studio kubwa ndani ya Mbeya iitwayo Makanta Records ndipo ilipofanikiwa kukutana na wasanii machachari watatu huku wakiwa wanajiita FLG.
Wasanii hao ni Fidelosso,Lastie bone na Goliath.Baada ya hapo NDT ikawauliza nia ya wao kujuinga na kuunda FLG na nini maana yake?,Goliath akajibu akisema "FLG ni kifupisho cha majina yetu wote watatu","Kwanza FLG siyo kundi,ila ni muunganiko wa muda mfupi kwa ajili ya 'project' tunayoifanya kwa sasa"alijibu Lastie Bone"Pia hatuna menejementi yoyote ni sisi wenyewe tumeamua kusimama na kufanya kitu hichi"aliongeza.
"Kwa upande wangu mimi bado niko MCB,na wala haiingiliani na FLG"Alijibu Fidelosso.
Lilipokuja swala la Goliath kuwepo Mbeya au kurudi Mwanza,yeye mwenyewe akadai kuwa bado yupo Mbeya kwani hajamaliza masomo yake ya chuo,hivyo ana muda mwingi wa kumuwezesha kufanya 'projects' nyingi zaidi.
"T-Block na Makanta bado ni viwanja vyangu vya nyumbani,hii 'project' ni binafsi tu na haimaanishi nimeamua kujitegemea" Aliongeza Lastie Bone.
FLG walielezea kuwa wameazimia kufanya  'project' hii ili iwafikishe hatua mpya katika muziki,na kwa sasa tayari wamekwisha fanya nyimbo nne,na zimebaki nne tu ili kukamilisha Albamu yao ambayo bado hawajaipa jina.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved