Tigo yadhamini mashindano ya mbio za Mbuzi jijini Dar



4
Vijana wakikimbiza Mbuzi ili kupata mshindi wa mbio hizo wakati wa tamasha la mbio za Mbuzi (Goat Race) lillilofanyika Dar es Salaam.
3
Vijana wakiingiza Mbuzi katika eneo la kukimbilia wakati wa tamasha la mbio za Mbuzi (Goat Race) lilofanyika jijini Dar es Salaam.
6
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo John Wanyancha (kushoto) akikabidhi hundi kwa mmiliki wa Mbuzi aliyeshinda, Mark Golding kutoka kampuni ya PM Group.
1
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, John Wanyancha akipata huduma katika banda la Tigo, wakati wa tamasha la mbio za mbuzi (Goat Race), zilizofanyika Jijini Dar es Salaam ili kukusanya pesa za kusaidia jamii.
2
Watoto wakicheza katika puto maalum la Tigo (Jumping Castle) wakati wa tamasha la mbio za Mbuzi (Goat Race) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwigulu na Wassira wakoleza mbio za Urais

MAKADA wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba na Stephen Wassira wametangaza rasmi nia yao ya kutaka kuwania kupitishwa na chama hicho, kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwigulu ambaye ni mbunge wa Iramba Mashariki, alitangaza uamuzi wake huo mjini Dodoma wakati Wassira alitangaza nia hiyo jana jijini Mwanza mbele ya viongozi, wanachama na waasisi wa TANU na CCM na wananchi.
Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa chuo cha Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kauli ya Wassira Akihutubia mamia ya wakazi waliofurika katika maeneo ya chuo hicho, alisema ameamua kutangaza nia yake hiyo kwa sababu anao uwezo mkubwa wa ndani na nje wa kuongoza nchi.
Pia, alisema amefanya hivyo ili kuvunja baadhi ya minong’ono kutoka kwa baadhi ya watu, iliyomtaka kutangaza nia hiyo. Aliainisha mambo makubwa matano, ambayo atayatekeleza endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.
“Niwashukuru sana kwa kuacha kazi zenu na mkaja hapa kushuhudia jambo hili muhimu, kwa zaidi ya mwaka mzima kumekuwepo na minong’ono kutoka kwa juu ya mimi kuwania urais, leo nimekuja hapa Mwanza kuvunja minong’ono hiyo na kutangaza wazi kuwa natangaza rasmi kuwania nafasi hiyo”, alisema.
Alisema ameamua kujitokeza kuwania nafasi ya urais, kwa kuwa yeye ni mtu sahihi kuongoza nchi. Alisema amefanya kazi kwa karibu na marais wote wa nchi hii, waliopita tangu awamu ya kwanza hadi ya sasa na kwamba alikuwa na fursa pekee ya kuwasiliana nao.
Aliongeza kuwa sababu nyingine iliyomsukuma kuwania nafasi hiyo ni kuwa anaijua vizuri Tanzania kwa kuwa ameshiriki katika siasa za nchi akiwa angali kijana mdogo wa umri wa miaka 25.
“Mwaka 1970 nikiwa na umri wa miaka 25 nilichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo langu la Mwibara wilayani Bunda na nimewatumikia watanzania katika nyadhifa nyingi za juu kwa miaka 45 iliyopita kwanza kama Mbunge, Mkuu wa mkoa, Naibu Waziri na baadaye Waziri kamili katika awamu mbalimbali”, alisema, na kuongeza,
“Baada ya tafakari ya muda mrefu na ya kina kwamba nimeamua ni sahihi, ni wakati mwafaka na kwa hakika, mimi ndiye mtu sahihi wa kujitokeza na kuwahudumia watu wa nchi hii “, alisema.
Vipaumbele vyake
Alitaja baadhi ya vipaumbele anavyotarajia kuvitekeleza katika Serikali yake, endapo watanzania watamchagua kuwa Rais kuwa ni kuteng’eneza nafasi za ajira kwa vijana, kujenga uwezo wa watanzania kushiriki kikamilifu katika ukuzaji wa uchumi, kuwekeza katika watu, ikiwa ni pamoja na kufumua upya mfumo wa elimu ili kuwezesha wafanyakazi kuwa na ushindani.
Wasira alivitaja vipaumbele vingine atakavyovitekeleza kuwa ni pamoja na kuwa na ujenzi wa miundombinu inayoendana na mazingira ya Karne 21, yenye dhamira ya kukuza uchumi wa nchi, kuwezesha ushiriki mpana wa demokrasia na maendeleo ya kiuchumi sanjari na utekelezaji wa mipango, Sera na mikakati mbalimbali ya kiserikali.
“Nitaendeleza utawala wa kikatiba, utawala bora na wa sheria, kujenga uchumi imara wenye kuleta ushindani na Serikali yangu itajengwa katika misingi iliyowekwa na awamu zilizotangulia, hasa kwa rekodi nzuri ya mtengamano wa uchumi mpana wa nchi na nitafanya marekebisho makubwa katika utumishi wa umma ili uendane na wajibu wake wa kuwatumikia watanzania”, alifafanua Wasira aliongeza kuwa endapo atachaguliwa kuwa Rais, serikali yake itaimarisha kilimo kwa kuleta mapinduzi makubwa ya kilimo na uchumi vijijini na kuondokana na kilimo cha jembe la mkono .
“Jembe la mkono sasa tutalipeleka kwenye jumba la makumbusho, hii itakwenda sanjari na kuwaunganisha wakulima wajiunge katika ushirika ili waweze kukopeshwa matrekta kwa ajili ya kuimarisha kilimo” alisema.
Aidha, alisema endapo atachaguliwa kuiongoza nchi, Serikali yake itaanzisha mjadala wa kitaifa wa kupambana na rushwa, ambapo aliweka bayana kuwa amekuwa ni miongoni mwa viongozi waadilifu waliotumikia nchi bila ya kupata na kashafa yoyote ile “Tutaanzisha mjadala wa kitaifa wa kupambana na rushwa, Baba wa taifa aliwahi kusema anayesema atapambana na rushwa, muangalie machoni kama ana ujasiri wa kupambana na rushwa”, alisema.
“Mimi sina rekodi ya kuwaibia watanzania, mlisikia katika EPA sikutajwa, sakata la Escrow nalo sikutajwa, sio kwamba mimi sifanyi kazi za madaraka, lahasha, Mimi ni Waziri wa Kilimo, ningeweza kuwaibia mbolea, na nimekaa Ikulu muda mrefu, hakuna biashara pale, mkimchagua mla rushwa angalieni atauza hadi Ikulu yenu,” alisema Wassir

Balozi Karume kutangaza nia leo

JOTO la urais wa awamu ya tano linazidi kupanda miongoni mwa makada wa CCM, baada ya baadhi yao kuanza kutangaza nia, na leo Balozi mstaafu Ali Karume anatarajiwa kufanya hivyo, akilenga kutaka kumrithi Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake Oktoba mwaka huu.
Balozi Karume ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, alisema anakusudia kutangaza nia katika ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kati, Dunga.
Akizungumza na gazeti hili, Karume alisema atajitosa katika kinyang'anyiro hicho ikiwa ni mara ya pili kufanya hivyo kwa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mara ya kwanza ikiwa mwaka 2010.
“Nakusudia kutangaza nia ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano kwa sababu sifa ninazo pamoja na uwezo wa kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema.
Balozi Karume ni mwanadiplomasia mstaafu ambaye alipata kushika nafasi za kuwa balozi wa Tanzania katika nchi mbali mbali duniani zikiwemo Marekani, Ubelgiji, Ujerumani na Italia ambako alistaafia kazi miaka minne iliyopita.
Wakati Karume akiwatarajiwa kuanika dhamira yake leo, Waziri wa zamani wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Amina Salum Ali naye anakusudia kuchukua fomu ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma wiki hii.
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita, alisema ameshawishika kuchukua fomu ya urais kutokana na nafasi na fursa zilizopo kwa wanawake kushika nafasi ya uongozi wa ngazi za juu.
Alisema huu sio wakati wa kuwaachia wanaume kufanya kila kitu na kujiamulia, kwa sababu wanawake wa Tanzania wamewezeshwa na kujengewa uwezo ambao sasa unatosha kuwafanya kushika nafasi za juu za uongozi.
“Msimamo wangu siku zote naamini kwamba mwanamke anao uwezo mkubwa wa kushika nafasi za juu za uongozi na ndio maana nimekuwa nikijitokeza kuwania nafasi hizo kadri inavyowezekana,” alisema.
Mwaka 2000, Amina ilikuwa mwanamke pekee aliyejitokeza kuwania katika kinyang'anyiro cha urais wa Zanzibar na kuibuka nafasi ya nne kwa kupambana na Rais mstaafu Abeid Amani Karume na Waziri kiongozi wa wakati huo Dk Mohammed Gharib Bilal ambaye sasa ni Makamu wa Rais wa Tanzania.
Mwanasiasa huyo mkongwe ambaye ni Balozi wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataifa (UN), aliwahi kuwa Waziri wa Fedha katika utawala wa Rais Dk Salmin Amour Juma 'Komandoo’, lakini, amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, chini ya utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi.
Wanadiplomasia hao, Karume na Amina wanakuwa Wazanzibari pekee hadi sasa kuonesha nia ya kuingia katika kinyang’anyiro cha urais wa Tanzania.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai alisema kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na chama, watu wanaokusudia kuchukua fomu kuwania nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watalazimika kwenda Dodoma, yaliko makao makuu ya chama hicho.

Marais EAC wataka uchaguzi wa Rais Burundi uahirishwe

WAKUU wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), wameitaka Burundi kuahirisha uchaguzi kwa takribani mwezi mmoja na nusu ili kurejesha hali ya amani nchini humo na kulitaka Bunge kusimamia mchakato huo.
Aidha, wametoa wito wa Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Mataifa (UN)na wadau wengine kuunga mkono juhudi za EAC katika kumaliza matatizo ya Burundi.
Akisoma maazimio ya viongozi hao yaliyofikiwa kwenye kikoa cha pili cha dharura cha kujadili hali ya Burundi kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa EAC, Dk Richard Sezibera alisema maamuzi hayo yanazingatia hali ilivyo nchini Burundi na kutaka kusogeza mbele uchaguzi ili kuweza kurejesha amani nchini humo.
“ Tunazitaka mamlaka zote nchini Burundi kuhakikisha inasitisha uchaguzi kwa muda usiozidi mwezi mmoja na nusu na kuliomba Bunge kusimamia uahirishwaji wa uchaguzi huo,” alisema.
Alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya wakuu hao kupokea taarifa ya mawaziri wa mambo ya nje na wanasheria wakuu au mawaziri wa sheria wa nchini wanachama, ripoti ya mwakilishi wa UN katika Ukanda wa Maziwa Mkuu na ile ya timu ya Wazee wa Jumuia ya Afrika Mashariki inayoongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba..
Uchaguzi wa Wabunge nchini Burundi ulipangwa kufanyika Juni 5 mwaka huu na ule wa rais uliopangwa kufanyika Juni 26. Hii ni mara ya pili kwa EAC kuagiza uchaguzi huo kusogezwa mbele, kwani katika kikoa cha kwanza waliagiza uchaguzi huo kusogezwa mbele kwa muda usiozidi kipindi cha uongozi uliopo madarakani.
Katika kikao cha jana kilichoanza saa 8:20 mchana na kumalizika saa 11:09, ambacho Rais Pierre Nkurunziza aliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Alain Nyamitwe, kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Uganda Yoweri Museveni, huku Rais wa Rwanda Paul Kagame aliwakilishwa na Waziri wa Jumuia ya Afrika Mashariki na Uhusiano Valentine Rugwabiza.
Pia kilihudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, Mwenyeikiti wa Kamishna ya AU, Dk. Nkosazana Dlamini Zuma huku Mwenyekiti wa Ukanda wa Maziwa Makuu, Eduardo Dos Santos aliwakilishwa na katibu wa jumuia hiyo, Profesa Ntumba Luaba.
Sezibera alisema pia EAC imeagiza vikundi vya vijana ambavyo vinaushirika na vyama vya siasa nchini Burundi kunyang’anywa silaha na kuitaka serikali kuweka mazingira mazuri ambayo yatawafanya wakimbizi kurejea nchini mwao.
Aidha, EAC imepongeza kurejea kwa utawala wa kikatiba nchini Burundi baada ya kutokea jaribio la mapinduzi. Akiwa Tanzania kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa kwanza wa EAC waliokutana Mei 13 kujadili mgogoro wa kisiasa nchini humo, majenelali wa juu wa nchi hiyo walifanya jaribio la kumpindua Rais Nkurunziza ambalo lilizimwa na majeshi ya nchi hiyo.
“ EAC inasikitishwa na hali ya nsitofahamu inayoendelea nchini Burundi. Tunawataka wadau kuacha vurugu na machafuko yaliyosababisha vifo, uharibifu wa mali na wengine kukimbia nchi yao.”
Machafuko yalianza nchini humo tangu Aprili 26, mwaka huu na kusababisha zaidi ya vifo 20, huku maelfu wakikimbia nchi yao, yametokana na hatua ya Rais Nkurunziza kutangaza azima ya kuwania muhula wa tatu wa uongozi, jambo ambalo linalalamikiwa na wapinzani kwa madai kuwa ni kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Urais 2015: Nchemba kutangaza nia leo

Naibu Waziri wa Fedha  mwigulu Nchemba.                                       Naibu Waziri wa Fedha mwigulu Nchemba.                              
Mwanasiasa Kijana  anayekuja juu katika medani za siasa nchini Tanzania ambaye pia  ni Naibu Waziri wa Fedha  mwigulu Nchemba anatarajia kutangaza nia ya kutaka kugombea urais mwaka 2015.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wake amebainisha kwamba  leo siku ya jumapili tarehe Tar.31.05.2015 Nchemba  atatangaza   nia ya kugombea urais katika na kusisitiza kuwa Mazungumzo yake na wananchi  yatajikita  katika kuomba ridhaa ndani ya Chama cha Mapinduzi ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Nchemba atazungumzia nia hiyo   majira ya   Saa 9 Alasiri hadi 12 Jioni   katika ukumbi wa Mwl.Nyerere “Hall “chuo cha Mipango mkoani  Dodoma .
Baada ya kuhakikisha kuwa haujapitwa katika tukio la kutangaza nia Mbunge wa Monduli Edward Lowassa leo Team nzima ya Mtandao wa Hivisasa itawasili tena mkoani Dodoma kukujulisha kila kinacho endelea,  endelea kuwa  nasi.
                 

Vigogo 5 TRL kupandishwa kizimbani kashfa ya mabehewa

    MAOFISA watano wa Serikali, wanatarajiwa kupandishwa kizimbani hivi karibuni, kutokana na kashfa ya uagizaji wa mabehewa 274 kutoka India, huku wengine wakitarajiwa kuchukuliwa hatua za kiutawala.
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, ameliambia Bunge jana kuwa Kamati Maalumu iliyoundwa na wizara yake, imemaliza kazi na kumkabidhi ripoti hiyo. “Hii ndio ripoti ya Kamati (akionesha kwa wabunge).
Wamenikabidhi ripoti juzi na iliundwa na watu wa Ofisi ya CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa) na wahandisi,” alisema Sitta.
Alikuwa akifanya majumuisho ya hoja za wabunge kuhusu makadirio ya bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2015/16, ambayo aliyawasilisha bungeni jana asubuhi na kupitishwa na Bunge baadaye mchana.
Waziri huyo mkongwe alisema kamati hiyo ilienda hadi Calcutta, India ambako mabehewa hayo 274 yalitengenezwa na kwa mujibu wake, mabehewa hayo si chakavu, kama ilivyodaiwa awali.
Hata hivyo alisema “kuna makosa mawili hapa ambayo ni uzembe wa pande mbili, waagizaji na watengenezaji. Kuna tatizo katika specification (vipimo). “Hapa kuna majina ya watu wote waliohusika katika suala hili.
Watano tunawapeleka mahakamani, wengine tutawachukulia hatua za kiutawala.” Aidha, aliweka bayana kuwa katika maofisa hao watano watakaopelekwa mahakamani, wawili ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mbunge huyo wa Urambo Mashariki alilazimika kusema hayo baada ya Kambi Rasmi ya Upinzani kudai kuwa Serikali imekithiri kwa ufisadi, akisema ufisadi unafanywa na watendaji.
“Kuweni makini sana mnapozungumzia suala la ufisadi na wizi, hili si suala jepesi. Ufisadi si suala la kubadili sura. Ufisadi ni njama za watendaji na halina vyama.
“Nataka kuwaambia kuwa kwenye hii shughuli ya reli (kashfa ya mabehewa), wapo watendaji wawili ambao ni wanachama wa Chadema. Ndio, subirini tukiwapeleka,” alisema Sitta na kuihoji Chadema kuwa inasema CCM kuna ufisadi je, inapomchukua mwanachama wa CCM, ufisadi unabadilika anapoingia kwao?
Akifafanua sakata hilo, alisema katika suala la vipimo limeonekana kuwa havikuzingatiwa kwani mabehewa hayana milimita za kutosha, hivyo kuwapo na matatizo katika ukataji wake na wakati treni ikiwa safarini.
Alisema kutokana na hilo, mtengenezaji ameitwa na yuko katika karakana nchini, ambapo kwa gharama zake anafanya marekebisho katika mabehewa hayo yaliyoanza kutoa huduma katika treni mwezi uliopita.
Aidha, Sitta alisema si kweli kuwa hasara iliyopatikana ni Sh bilioni 200, bali ni Sh bilioni 12 na wote waliohusika watachukuliwa hatua stahili. “Pia tumemwomba Mwanasheria Mkuu ili sehemu ya hasara hii ibebwe na mtengenezaji na nyingine itabebwa na Serikali kutokana na uzembe uliofanyika,” alisema Sitta.
Waziri huyo alilazimika kusema hayo baada ya baadhi ya wabunge kumjia juu, wakitaka eleze kwa kina nini kimetokea uagizaji huo wa mabehewa uliofanywa wakati wa utawala wa Waziri Dk Harrison Mwakyembe.
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alisema ufisadi huo ni zaidi ya kashfa ya Richmond na kuwa Waziri husika, Katibu Mkuu na Katibu Mkuu Hazina, walipaswa kujiuzulu mara moja.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kashfa hiyo inaendeleza ufisadi uliotamalaki serikalini na kumtaka Sitta aweke bayana hatua alizochukua.
Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi (Chadema), Haroub Mohamed Shamis (CUF), pia walizungumzia hilo. Aidha, Sitta aliahidi kufuatilia ripoti ya CAG kuhusu uuzwaji wa nyumba za Mamlaka a Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) jijini Dar es Salaam na Mbeya.
Mapema mwezi uliopita, Sitta alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Kipallo Kisamfu na wengine wanne, ili kupisha uchunguzi wa kashfa ya uingizaji wa mabehewa feki ya mizigo.
Wengine waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa Mitandao, Ngosomwile Ngosomiles, Mhasibu Mkuu, Mbaraka Mchopa, Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Jasper Kisiranga na Meneja Mkuu wa Manunuzi, Ferdinand Soka.
Alisema mabehewa mabovu yaliingizwa nchini mwaka jana kupitia kandarasi ya Kampuni ya M/S Hindustan Engineering and Industrial Limited ya India, ambayo ililipiwa asilimia 100 ya gharama zote ambazo ni Sh bilioni 230.
Alitoa wiki tatu kuanzia Aprili 20, mwaka huu kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi wa sakata hilo.

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi.
Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki.
Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo.
Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa linaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi.
“Maofisa ardhi lazima mfanye kazi kwa kuzingatia taratibu ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima ambayo inatokea miongoni mwa wananchi na kuwasababisha kuichukia serikali yao,” alisema Lukuvi.
Alibainisha kwamba mtumishi yeyote wa idara hiyo atakayebainika kukiuka taratibu atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu na sheria za kazi na zile za nchi.

Lowassa aanza safari yake

ALIYEKUWA Waziri Mkuu, Mbunge wa Monduli mkoani Arusha, Edward Lowassa, ametangaza nia ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili awe mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lowassa alitangaza nia hiyo katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid, uliofurika watu waliokusanyika uwanjani hapo tangu saa 12 asubuhi wakimsubiri mtangaza nia huyo, aliyeingia uwanjani hapo kwa mbwembwe saa 9 mchana.
“Nina ari, shauku na uwezo wa kuongoza Tanzania. Hatumtafuti Rais tu, bali tunamtafuta Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti wa CCM. “Tunamtaka mzee mzoefu, mwenye ukomavu wa kisiasa aliyekaa ndani ya chama miaka ya kutosha na kukifahamu chama hiki,” alisema Lowassa.
Akizungumza katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na televisheni na redio kadhaa nchini, Lowassa alisema Watanzania wanahitaji mtu wa kuwaongoza kujenga Taifa imara.
Amesema Taifa hilo ni ambalo kila mwananchi wake anapaswa kuishi akiwa na uhakika wa usalama wa maisha yake, mali zake na mahitaji yake muhimu huku akijiridhisha kwamba leo yake ni bora kuliko jana yake.
Kwa mujibu wa Lowassa, Watanzania wanataka mabadiliko na wanaendelea kuamini kwamba CCM ina uwezo wa kusimamia mabadiliko hayo.
Hata hivyo, alikumbusha wosia wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, alioutoa kwa wanaCCM mwaka 1995 wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Kwanza wa Mfumo wa Vyama Vingi kuwa: “Watanzania wasipopata mabadiliko ndani ya CCM, watayafuata nje ya CCM,” alinikuu hotuba hiyo na kusema ana uhakika na hana shaka CCM ina uwezo wa kuwapa Watanzania mabadiliko.
Lowassa aliweka wazi misingi mikuu ya utendaji wa Serikali atakayoiongoza, ikiwa CCM itampa ridhaa ya kugombea urais na wananchi wakimchagua kuwa Rais wa Awamu ya Tano.
Kwanza amesema ataongoza Serikali inayozingatia uwajibikaji, ambapo alidai kuwa Watanzania wanamfahamu yeye si mtu wa maneno, ni mtu wa vitendo.
Amesema anaamini kabisa kuwa hakuwezi kuwa na uongozi imara, utakaoweza kusimamia ujenzi wa Taifa imara, iwapo hakutakuwepo ujasiri wa kuwajibika.
Malengo yake Lowassa aliyekuwa akikatishwa hotuba zake kwa shangwe na kurudia rudia maneno kwa matakwa ya wananchi, alisema pamoja na kuwa Ilani ya CCM iko mwishoni ambayo itaelekeza Serikali inachopaswa kufanya, lakini mgombea pia anaruhusiwa kusema anachoamini.
Katika anayoyaamini, Lowassa alisema ataimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa kuimarisha misingi yake na kulinda misingi muhimu ya Muungano ya undugu wa damu na kihistoria, uliojengwa na waasisi Mwalimu Julius Nyerere na Shekhe Abeid Aman Karume pamoja na kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar.
Lowassa aliahidi kupambana na hisia za udini na ukabila na kuimarisha siasa za uzalendo, huku akijenga uchumi wa kisasa na shirikishi utakaonufaisha Watanzania wote wa mijini na vijijini.
Mtangaza nia huyo, pia ameahidi kuondoa alichokiita sifa mbaya ya kuomba huku akisema kuwa anachukia sana umasikini, kwa kuwa kwa wingi wa rasilimali za Tanzania, ikiwemo mito na maziwa na ardhi kubwa, ataibadilisha nchi kuwa mkoba wa neema.
Katika ukuaji wa uchumi, Lowassa alisema atahakikisha ukuaji huo unaenda sambamba na upatikanaji wa haki za huduma muhimu kwa wananchi, ikiwemo huduma za afya na maji safi na salama.
Kwa mujibu wa Lowassa, marais waliotangulia kuanzia Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Nne, Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Kikwete anayekaribia kumaliza muda wake, wamefanya kazi nzuri lakini kuna nafasi ya kufanya vizuri zaidi.
Lowassa alisema katika fursa hiyo ya kufanya vizuri zaidi, ameazimia kuanzisha alichoita kuwa ni mchakamchaka wa maendeleo, huku akisema pia atapambana na rushwa kwa kuwa bila kupambana na rushwa, huduma na haki kwa wananchi hazitapatikana.
“Hatuwezi kujenga uchumi wa kisasa kama rushwa itatawala na Serikali haitatawala vizuri kama rushwa itaendelea kuwepo,” alisema.
Uwekezaji wa nje
Alisema Tanzania ya sasa imekuwa ni miongoni mwa nchi zinazovutia uwekezaji mkubwa katika sekta ya gesi ambayo inatajwa kwamba inaweza kuja kubadilisha kabisa maisha ya Watanzania.
Hata hivyo, alisema katika kipindi hicho kuelekea ujenzi wa uchumi wa kisasa, kimeibua hofu na wasiwasi miongoni mwa wananchi kwamba hawatanufaika na ukuaji huo wa uchumi na ugunduzi wa utajiri mkubwa wa gesi asilia.
Lowassa alisema vijana wanataka kuona ukuaji wa uchumi na ugunduzi wa utajiri huo unakwenda sambamba na uzalishaji wa ajira zenye maana, ili wakabiliane na changamoto za maisha yao.
Akizungumzia uongozi imara na Taifa imara, alisema Urais si kazi ya lelemama na inahitaji utashi na hata kabla ya kushawishiwa na wenzako, ni lazima kwanza wewe mwenyewe uamini na uwaaminishe wenzio kwamba unao uwezo wa kuwaongoza wananchi wenzako.
Mambo ya kujivunia
Alisema ana mambo ya kujivunia ikiwa ni pamoja na kushiriki katika vita ya Kagera ya kumng’oa Iddi Amini akiwa askari wa mstari wa mbele na kutokana na rekodi hiyo, anaamini kuwa ana sifa za kuwaongoza Watanzania katika zama mpya za ujenzi wa Taifa la kisasa.
Mbali ya Taifa la kisasa pia lenye watu wazalendo, walioshikamana na lenye uchumi imara unaomnufaisha kila Mtanzania, amesema kuwa anao uwezo wa kuwapa Watanzania uongozi imara kwa ajili ya ujenzi wa Taifa imara na hiyo ndio safari ya matumaini.
Kingunge
Naye mwanasiasa mzoefu, Kingunge Ngombale Mwiru alisema kuwa Waswahili walinena kuwa ‘’mzigo mzito mpe Mnyamwezi’’ na yeye anasema ‘’mzigo mzito mpe Lowassa.” Kingunge alisema Lowassa ameanzisha safari ya kuelekea Ikulu hivyo wote na kwa niaba ya wazee wenzake watamuunga mkono katika safari hiyo ya matumaini bila wasiwasi wowote.
Alisema nchi inahitaji kiongozi bora mchapakazi na mwenye uthubutu hivyo sifa zote hizo anazo Lowassa na aliwataka wakazi wa Arusha na nje ya Arusha kumuunga mkono mgombea huyo wa CCM.
Alisema asilimia 30 ya Watanzania wana umasikini sugu wa kupindukia na hakuna mabadiliko katika awamu zote hivyo Lowassa anahitajika apambane na hali hiyo na ikiwezekana amalize ama apunguze.
‘’Ninamshukuru na kumpongeza Lowassa kwa kutangaza nia yake ya kuelekea Ikulu hivyo anapaswa kuungwa mkono kwa hali na mali.’’‘’Huu umati uliokuja hapa kutoka kila kona ya nchi kuja kumsikiliza Lowassa sijawahi kuona kwani mara ya mwisho niliuona wakati tunamsubiri Mwalimu Nyerere arudi kutoka Umoja wa Mataifa kuleta Uhuru,” alidai.
Wanaofuata
Baada ya Lowassa jana kutangaza nia, leo itakuwa zamu ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira atakayetangazia nia jijini Mwanza kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba naye atatangazia nia yake mkoani Dodoma kwenye Chuo cha Maendeleo ya Mipango, eneo la Msalato.
Wanachama wengine wa CCM watachukua fomu wiki ijayo kuanzia kesho akiwamo mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Charles Makongoro Nyerere, William Ngeleja, Profesa Mark Mwandosya na Bernard Membe.
Mbali ya hao, orodha inayotajwa inawahusisha Lazaro Nyalandu, Amina Salum Ali, Dk Hamis Kigwangalla, Dk Titus Kamani, Shamsi Vuai Nahodha, Dk Emmanuel Nchimbi, January Makamba, Frederick Sumaye, Profesa Sospeter Muhongo na Dk Asha-Rose Migiro.

Wabunge Afrika Mashariki wawe bora



WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe amependekeza mfumo wa kupata wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania ubadilishwe.
Waziri huyo aliyasema hayo juzi alipokuwa akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha wa 2015/2016 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, ipo haja ya kubadili mfumo wa kupata wabunge hao kutoka Tanzania, hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa Bunge la Afrika Mashariki ndicho chombo kikuu cha kutunga sheria za jumuiya.
Waziri anafafanua zaidi kuwa sheria hizo kwa mujibu wa Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya, zinapewa nguvu juu ya sheria za nchi wanachama katika masuala ya utekelezaji wa mkataba huo.
Anasema wajumbe wa bunge hilo wanaruhusiwa kimkataba kuwasilisha hoja na miswada binafsi bungeni kwa majadiliano na uamuzi, lakini fursa hiyo imetumiwa vizuri na wawakilishi wa baadhi ya nchi wanachama kwa maslahi mapana ya nchi zao kuliko ilivyo kwa wawakilishi wa Tanzania.
Mbali ya hilo Waziri Mwakyembe anasema kutokana na hali hiyo kuna umuhimu wa Watanzania kuacha mfumo wa sasa wa kuwapata wabunge hao na kuangalia mfumo utakaopeleka watu watakaokuwa wazalendo na watakaotetea maslahi ya Tanzania, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa dhati kabisa tunaungana na Waziri Mwakyembe katika kupendekeza mfumo unaotumika sasa katika kuwapata wabunge hao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ubadilishwe haraka iwezekanavyo kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
Kama alivyosema Waziri na kama inavyofahamika, utaratibu wa kuwapata wabunge wa Afrika Mashariki umekuwa hauna tija kwa maslahi ya Taifa letu na kwa muda mrefu umekuwa ukilalamikiwa kutawaliwa na rushwa na ushabiki zaidi kuliko kuangalia vigezo vya utaalamu na elimu kwa wahusika.
Hatua ya kukosekana kwa sifa kwa wabunge wanaochaguliwa kwenda kuliwakilisha Taifa kwenye jumuiya hii muhimu katika ukanda wa Afrika Mashariki ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu kwani kuna uwezekano mkubwa wa maslahi ya Tanzania kutozingatiwa ipasavyo.
Kama inavyofahamika, jumuiya za kikanda ni maeneo yanayopewa msukumo mkubwa katika diplomasia ya dunia ya leo, ambapo mataifa yote duniani yamekuwa yakipeleka nguvu katika kuvijengea uwezo vyombo vyake vya uwakilishi katika kanda zao kufahamu namna ya kushindana na kutetea maslahi ya mataifa yao ndani ya kanda zao.
Kutokana na changamoto hii ya wabunge wetu wa Afrika Mashariki kuchaguliwa kwa rushwa bila kuwa na sifa ni vigumu kuwapata wawakilishi wenye uwezo na uelewa mpana wa kufahamu namna ya kujenga hoja katika Dunia ya leo yenye kuelemea zaidi kwenye ushawishi wa Diplomasia ya Uchumi jambo ambalo ni la hatari kwa Taifa letu.
Ni lazima sasa suala la upatikanaji wa wabunge wa Afrika Mashariki, likatazamwa upya ili wabunge watakaochaguliwa wawe na uwezo mkubwa wa kujenga hoja mbele ya wabunge wengine kutoka nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya, nchi ambazo zinaonekana wazi zimepania kutumia fursa za ndani ya jumuiya kutetea maslahi ya mataifa yao.
Kwetu sisi tunaona kwamba bado hatujachelewa. Bado tunao muda wa kurekebisha kasoro zinazojitokeza katika kuwateua wawakilishi wetu kwenye jumuiya za kikanda ili kuhakikisha kuwa tunapata maslahi kama ambavyo malengo yetu ya kujiunga yanavyojieleza

Yanga sasa wasaka mrithi wa Msuva

KLABU ya Yanga inajiandaa na maisha ya bila mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara Simon Msuva ambaye alifanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Kocha Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa aliliambia gazeti hili jana kuwa Msuva atajiunga na klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini na wao kama makocha lazima watatafuta mtu wa kuziba nafasi yake.
Kama Msuva ataondoka Yanga atakuwa mchezaji wa pili baada ya Mrisho Ngassa kutimkia kwenye klabu ya Free State ya Afrika Kusini na benchi la ufundi la Yanga likamsajili winga Deus Kaseke kuziba nafasi ya winga huyo wa kimataifa wa Tanzania.
“Kama hivyo Msuva anaondoka lazima tutasajili mtu kuziba nafasi yake, hivyo kila usajili tutakaofanya utalenga katika kuangalia mapungufu ya timu yetu,” alisema Mkwasa.
Alipoulizwa na mwandishi wa gazeti hili kama ofa ya kumtaka mfumania nyavu huyo ambaye alienda kufanya majaribio Afrika Kusini mwezi uliopita ishawafikia Mkwasa alisema kuwa kwa kuwa alienda kufanya majaribio lolote linaweza kutokea na wao lazima wajiandae kwa hilo.
Tayari benchi la ufundi kwa kushirikiana na Kamati ya Usajili ya klabu hiyo ishawapa mikataba wachezaji Kaseke kutoka Mbeya City, Haji Mwinyi kutoka KMKM ya Zanzibar na kipa chipukizi Benedict Tinocco kutoka Kagera Sugar.

Viongozi wa Afrika Mashariki kukutana kuijadili Burundi

Viongozi wa jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana hii leo mjini Dar es Salaam nchini Tanzania kuujadili mgogoro wa Burundi. Chini ya uenyekiti wa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, viongozi hao kutoka Kenya, Rwanda, Uganda na Burundi wanakutana kwa mara ya pili mwezi huu kujaribu kuutafutia ufumbuzi mzozo wa kisiasa wa Burundi ambayo imetumbukia katika msukosuko baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza atagombea muhula wa tatu. Uamuzi huo umesababisha maandamano ya umma ambayo yamedumu kwa miezi miwili na pia yalisababisha jaribio la mapinduzi lililoshindikana. Na katika kadhia nyingine, naibu wa mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Burundi Spes Caritas Ndironkeye na afisa mwingine wa tume hiyo wamekimbia nchini na hatma ya uchaguzi wa bunge unaotarajiwa Ijumaa hii ikiwa haijulikani.

Magazeti ya Tanzania leo May 31 2015 na stori zake kubwakubwa za michezo hardnews na dini.

Ungana na mimi tena kwenye post hii ya Magazeti, post maalum ambayo huwepo hapa New Day Taarifa kila siku kwa ajili ya kuyasogeza karibu yako Magazeti mbalimbali ya Tanzania na habari zake kubwakubwa kwenye kurasa za mwanzo na mwisho.DSC03108DSC03110                                                                                                                                                                    DSC03112                                                                                                                                                               DSC03113                                                                                                                                                                   DSC03114                                                                                                                                                                  DSC03115                                                                                                                                                                   DSC03116                                                                                                                                                                   DSC03117                                                                                                                                                                   DSC03118                                                                                                                                                                  DSC03119                                                                                                                                                                   DSC03120                                                                                                                                                                       DSC03122                                                                                                                                  DSC03124                                                                                                                                                                                                       DSC03137                                                                                                                                                               DSC03138                                                                                                                                                       DSC03140                                                                                                                                          DSC03126                                                                                                                                                         DSC03127                                                                                                      DSC03135                                                                                                                                                                                                                                                                                                             

Flaviana Matata kwenye tangazo jingine tena New York Marekani.

Ni Watanzania wengi sasa hivi yanatambua uwepo wa Mwanamitindo Flaviana Matata ambaye anaishi na kufanya kazi New York Marekani na amekua akiiwakilisha nchi yake vizuri tu pamoja na kuikumbuka kwa kusaidia kulipa ada za Wasichana wasiokua na uwezo            Good news ya leo ni Mwanamitindo huyu kuendelea kushine kwenye matangazo ya kibiashara na time hii kafanya hili tangazo la mavazi ya majira ya joto na kafanya na New York and Company.IMG_6388IMG_6389Picha zimetoka 8020fashionsblog.com

Waziri Nyalandu na mkewe Faraja kwenye jarida la bang time hii !

ba1                     Bang ni miongoni mwa Majarida ya Tanzania ambayo yamekuwepo kwenye headlines kwa muda mrefu ambapo time hii kuna toleo jipya ambalo Waziri wa mali asili Lazaro Nyalandu na mke wake ndio wamecover. Humo ndani wanazungumzia maisha yao, pia Waziri anazungumzia ishu yake ya kuutaka Urais wa Tanzania, amewazungumzia vijana wa Tanzania na mengine mengi hivyo ukiipata nakala yako utakutana pia na wengine akiwemo mtangazaji Sporah.bang

Ni Urais 2015 Tanzania… mengine ya January Makamba yako hapa.

January 2                Tume ya taifa ya uchaguzi imeshatangaza kwamba uchaguzi mkuu utafanyika October 2015 ambapo sasa ni headlines zake zinachukua nafasi kwa watu mbalimbali kutangaza nia za kugombea nafasi ya juu ya Urais. Post hii inamilikiwa na January Makamba ambae ni Mbunge wa Bumbuli Tanga na anautaka Urais pia ambapo May 30 2015 aliandika >>> ‘Wiki ijayo tutataarifu ni lini na kwa namna gani tutazungumza na Watanzania, kuchukua fomu, kuanza safari za mikoani kukutana na Watanzania

Waandishi wa habari wana kera kuchanganya lugha


NILIWAHI kusema hapa siku za nyuma kuwa bado ninavutiwa na nitaendelea kuvutiwa na watangazaji wa vipindi vya michezo na watangazaji wa mpira wa zamani kuliko wa kizazi hiki, ambacho bado ninaweza kusema kimeshindwa kukonga nyoyo za wadau.
Kuna tatizo kubwa kwenye kuandaa vipindi vya michezo kwenye radio mbali mbali na luninga hapa nchini pamoja na kutangaza matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ingawa teknolojia inakibeba kizazi hiki, lakini tumeshindwa kutumia vyema nafasi hiyo.
Zamani hakukuwa na runinga ila ulikuwa ukisikiliza mpira wa miguu kupitia Radio Tanzania ulikuwa unadhani kama uko uwanjani vile au unautazama moja kwa moja kwenye runinga kumbe ulikuwa unasikiliza kwenye redio. Haya tuachane na hayo, leo hii ninataka kuzungumzia suala moja tu la lugha kwa watangazaji wetu wa mpira na vipindi vya michezo wa kizazi hiki, pamoja na watu wapya kabisa kwenye utangazaji wa mpira na vipindi vya michezo.
Hawa wenyewe wanawaita wachambuzi. Yaani wenyewe hawawezi kutangaza au kuchambua mchezo kwa lugha moja tu ya Kiswahili, lazima wataingiza kiingereza katikati hadi inakera tena sio kidogo na mbaya zaidi wakiongea hicho kiingereza chao hawatafsiri hata kidogo na wakati mwingine utamsikia huyo mtangazaji au mchambuzi akiongea sentesi nzima ya kiingereza na baadaye anaendelea tena kwa Kiswahili, hapo ninakosa jibu kabisa.
Sasa ninajiuliza hiyo redio au runinga anayofanyia kazi imesajiliwa kurusha matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili ila yeye anajimwaga tu kwa kiingereza, kwa nini hasa?
Na wahusika wapo wapi au nao wanaridhishwa na hali hiyo. Miaka ya nyuma watangazaji walifanya kazi vizuri, tena sana na walijijenga kwa kupitia lugha hiyo hiyo ya Kiswahili na hawakuwa na mbwembwe kama zenu za kuingiza lugha ngeni kwenye matangazo yenu, inakera tena sio kidogo.
Mtu anayefanya hivyo sio kana kwamba hajui kiswahili, anakijua vizuri kweli kweli kwa sababu si tumekua naye uswahilini na tunaishi naye huko jamani ila akifika kwenye kipaza sauti tu, basi yeye ni mtu wa yes and no kama hakijui vile Kiswahili.
Mtu huyo huyo ukimpeleka kwenye matangazo ya lugha ya kiingereza tupu hicho kitakachozunguzwa mdomoni mwake utaomba maji ya kunywa ila kwenye matangazo ya Kiswahili lazima atie maneno ya kiingereza, inakera jamani.
Ndugu zangu jueni kuwa vituo mnavyofanyia kazi vimesajiliwa kwa kurusha matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili pia watazamaji wenu au wasikilizaji wenu walio wengi hawajui hiyo lugha mnayoichombeza mara kwa mara kwenye matangazo yenu ya vipindi vya michezo au ya mpira ya moja kwa moja.
Ninaamini na nina hakika hakuna neno lolote la kiingereza ambalo halina maana kwa lugha ya Kiswahili hata hizo sheria na kanuni za soka zimetafsiriwa kwa lugha mbali mbali, ikiwemo hicho Kiswahili ambacho nyinyi mnakiona kama hakina thamani.
Nimekuwa nikitazama na kusikiliza matangazo ya moja kwa moja ya ligi kuu Tanzania bara iliyomalizika wiki moja iliyopita na moja ya kitu ambacho nilikuwa ninakerwa nacho tena kwa kiasi kikubwa ni hicho cha hao wachambuzi hasa hasa kuingiza maneno ya kiingereza kwa kiasi kikubwa kwenye kuuchambua mchezo husika.
Kwa kweli kwangu mimi ninaona kama ni umbumbumbu na kukosa uelewa tu wa mtu anayefanya hivyo na hilo limekuwa ni tatizo kubwa kwa watu wanaofanya hiyo kazi kwa sasa, yaani anatia neno la kiingereza hata sehemu ambayo unaona kabisa ina neno zuri tu kwa Kiswahili ila lazima aweke huo upuuzi wake.
Mwalimu wangu mmoja wa mambo ya utangazaji wa mpira wa miguu aliwahi kuniambia matangazo ya mpira yanavutia na kuleta ladha kubwa kwa msikilizaji au mtazamaji yanapotangazwa na mtu mzawa wa lugha husika hapa alikuwa na maana kama mtu anayetangaza mpira kwa Kiswahili itakuwa vyema akiwa mswahili mwenyewe yaani lugha yake ya asili ni kiswahili.
Aliendelea kusema kuwa kuna maneno mengine ya soka yanaeleweka na kuwavutia wale wenye lugha yao ya asili, kwa mfano unaweza kusema Mrisho Ngassa anapigwa daruga pale au mpira umeingia kwenye Kamba akiwa na maana mpira umeingia kwenye nyavu kwa maana hiyo kama wewe Kiswahili chako ni cha kujifunza unaweza usielewe haraka haraka au itachukua muda kuweza kuelewa maneno ya kisoka kwenye Kiswahili ila ukiwa mzawa utayajua na utafurahishwa nayo.
Hayo ni machache tu na ndio maana kila mtu au shabiki wa soka anavutiwa na matangazo ya mpira pale yanapotangazwa kwa lugha yake ya asili kwa sababu anaielewa vilivyo kushinda lugha ya kigeni, sasa ninawashangaa nyie mnaopenda kuingiza maneno ya kiingereza kwenye matangazo ya mpira na vipindi vya michezo huku lugha yenu ya asili ni Kiswahili.
Mbona Kiswahili kina maneno matamu sana na ya kuvutia tena yanapendwa sana na mashabiki wa soka ambao wengi wao wanawasikiliza na kuwatazama nyie kila kukicha ingawa mnajiona kama hamkijui vile kumbe ovyo kabisa wakati mmezaliwa na kukulia nchini Tanzania.
Nipo hapa China kwa muda mrefu kidogo sasa ila sijawahi kusikia mtangazaji au mchambuzi wa soka akiingiza maneno ya lugha ngeni au ya kiingereza kama watangazaji na wachambuzi wetu wa bongo na wanajivunia lugha yao kweli kweli sasa sijui sie watangazaji na wachambuzi wetu wamelogwa na nani.

Makundi ya uzalishaji mali yatambuliwa


WIZARA ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa kushirikiana na halmashauri nchini, imetambua makundi 828 ya vijana waliojiajiri katika kilimo kwa lengo la kuwapa ushauri na mafunzo ya kilimo bora na cha kibiashara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Dk Mary Nagu, aliyasema hayo jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Felista Bura (CCM).
Katika swali lake, Bura alisema wapo vijana waliomaliza vyuo vikuu na kuamua kujiajiri katika kilimo, je, Serikali imekwishawatambua na kama iko tayari kuwakopesha pembejeo kama vile trekta bila wao kuwa na dhamana.
Dk Nagu alisema Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa Mkakati wa Taifa wa Vijana kujiajiri katika Sekta ya Kilimo(NSYIA).
“Mkakati huo umezingatia kwa makini Sera, Mikakati na Programu mbalimbali za kitaifa kuhusu maendeleo katika sekta ya kilimo na fursa za ajira zilizopo,” alisema.
Alisema kwa kuzingatia changamoto ya upatikanaji wa mikopo kwa vijana katika mabenki, Wizara inaendelea na mpango wa kuwasaidia vijana kupata mikopo yenye riba nafuu kupitia Mfuko wa Taifa wa Pembejeo.
Pia kutoa mafunzo kwa vijana kuanzisha vikundi vya vijana wanaoshiriki katika kilimo na kuvisajili sambamba na kuanzisha maeneo ya kilimo yaliyopimwa ili wapate mikopokatika benki.
Akijibu swali la nyongeza la Bura, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibuna Bunge), Jenista Mhagama alisema wapo vijana ambao tayari wamekopeshwa akitoa mfano wa kikundi cha Youth Foundation cha Ngara, Kagera ambacho kimekopeshwa Sh milioni 30.
Alizitaka Halmashauri nchini kuratibu vikundi hivyo vya vijana na kuviombea fedha kutokakwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambayo inalo fungu la kusaidia maendeleo ya vijana nchini.

Mgosi arejea Simba SC


KLABU ya Simba imezidi kujiimarisha baada ya kuwasajili wachezaji wawili, kipa wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Mohamed Abraham Mohamed na kumrejesha nyumbani mkongwe Mussa Hassan ‘Mgosi’.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hanspoppe, Abraham amesaini mkataba wa miaka miwili wakati Mgosi amesaini mkataba wa mwaka mmoja.
Usajili huo utatimiza jumla ya wachezaji watano baada ya kuwasajili Peter Mwalyanzi, Mohamed Faki na Samil Hajji Nuhu.
Aidha, usajili wa kipa huyo utaongeza idadi ya wale waliopo kufikia wanne, ambao ni Ivo Mapunda, Hussein Sharrif ‘Cassillas’na Peter Manyika.
Kuhusu usajili wa Mgosi, Hanspoppe alisema kuwa amemrejesha tena mchezaji huyo Simba baada ya kuonesha juhudi alipokuwa akiitumikia Mtibwa Sugar msimu uliopita.
Alisema bado ni mchezaji mwenye kiwango kizuri wakaona kuwa si vibaya kumrejesha nyumbani kwani ndiko alikotoka na kufanya vyema misimu iliyopita hivyo kuamini huduma yake inaweza kuwasaidia kujeresha kiwango cha timu.
“Ni kweli tumemsainisha Mgosi, ni mchezaji wetu wa zamani na amekuwa akifanya vizuri, tuna imani naye ndio maana tumempa tena nafasi ya kutusaidia,”alisema.
Mgosi alisajiliwa na Simba mwaka 2005 kutoka Mtibwa Sugar na mwaka 2012 aliuzwa DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alikocheza kwa misimu miwili na mkataba wake ulipokwisha akasaini timu yake ya zamani Mtibwa Sugar.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amesajiliwa Simba baada ya kumalizika kwa mkataba wake Mtibwa Sugar hivi karibuni.
Mgosi wakati anahojiwa jana asubuhi na kituo kimoja cha redio, alisema hajasaini isipokuwa amezungumza na kufikia hatua ya kusaini hivyo yuko mbioni kuja Dar es Salaam kumalizana na Simba, kauli ambayo ilionekana kupishana na ile ya Hanspoppe aliyethibitisha kuwa tayari wameshamsajili mchezaji huyo.
Usajili huo wa Hassan unaonesha dhahiri kuwa, Simba wanaifuata Yanga kwa kuwa na wachezaji wenye umri mkubwa, wakati sera yao ilikuwa ni kusajili chipukizi, ambao wataichezea timu hiyo kwa muda mrefu.
Naye mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Collin Frich alisema Mgosi ni mchezaji sahihi kwao na ana uwezo na kiwango chake kipo juu ndio maana wanataka kumrejesha kikosi.
Mgosi akiwa Simba aliwahi kuisaidia timu hiyo kufuzu mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Tusker mwaka 2005 baada ya kuifungia mabao mawili dhidi ya SC Villa ya Uganda akitokea benchi katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Katika msimu uliopita, Mgosi alizifunga Simba na Yanga, ambapo katika mabao yake matatu, mawili amevifunga vigogo hivyo.

La kukamatwa kwa viongozi FIFA Tanzania tusilipuuze


                                                                                          MOJA ya habari kubwa zilizotawala vyombo vya habari wiki hii, ni sakata la kukamatwa kwa viongozi wa ngazi ya juu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Viongozi hao walikamatwa wakituhumiwa kushiriki katika suala la ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo kwa njia mbalimbali kama vile kupokea rushwa, kuzungusha fedha chafu na mengineo.
Kukamatwa kwao huko kumezua gumzo karibu kila kona ya dunia, hasa ikizingatiwa kuwa jana ilikuwa ni siku ya Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo ili kumpata rais.
Marais mbalimbali pamoja na viongozi wakubwa wa nchi mbalimbali wameshatoa misimamo yao kuhusu suala hilo, ambapo wapo waliosema kuwa ni sawa wahusika kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria vya nchi zao, huku wengine wakiona ni sawa na kuwa wangeachwa kumaliza suala lao FIFA.
Binafsi naona kuna mengi ya kujifunza katika suala hilo, kwanza ni kuona kwa kiasi gani katika soka, ambavyo rushwa imekithiri pia, suala ambalo ni la kupigwa vita.
Kwa muda mrefu FIFA imekuwa ikituhumiwa kujihusisha na mambo ya rushwa ila imekuwa ikisisitiza kuwa mambo yao yanajadiliwa katika ngazi ya shirikisho hilo.
Hata Sepp Blatter ambaye amekuwa akiliongoza shirikisho hilo kwa miaka mingi, mbali na kukamatwa kwa viongozi hao na kupelekwa kwenye mamlaka za nchi zao kwa maamuzi zaidi ya kisheria, amewatetea na kusema kuwa mamlaka hizo hazitakiwi kuingilia shughuli za soka kwa kuwakamata huku akitaka suala hilo kujadiliwa na wao wenyewe.
Hali kama hiyo imekuwa ikiathiri hata mashirikisho mengine yanayofanya kazi chini ya shirikisho hilo, hiyo ni kwa kuwa wapo watu ambao wamekuwa wakiiba fedha za mashirikisho ya soka kwenye nchi zao na wamekuwa wakijadiliwa katika mashirikisho na hakuna hatua za kisheria zinazochukuliwa.
Hiyo imekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya soka kwa kuwa hutumia hiyo ni kama kivuli cha kujificha dhidi ya ubadhirifu wao na kujikuta wakiathiri maendeleo ya soka.
Kwa kukamatwa tena kwa viongozi wa juu wa FIFA wakituhumiwa kuhusika na rushwa ni dhahiri kuwa kuna rushwa kwenye tasnia hiyo na tena hakuna haja tena ya kuendelea kulindwa eti kwa kusema kuwa masuala ya soka hayajadiliwi mahakamani
Hata kama bado hiyo ndiyo sera, lakini kwa wale wanaokamatwa kuhusika na rushwa au ubadhirifu wowote, basi ni muda umefika wa kuanza kuwakamata sio kuwaacha wakiendelea kufanya ubadhirifu kwa mgongo wa kanuni hiyo ya FIFA ya kuzuia masuala kama hayo kwenda mahakamani.
Yapo makampuni mbalimbali ambayo yamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia soka ambayo yanaweza kujitoa kutokana na uzembe wa watu kushindwa kusimamia vema majukumu yao.
Mfano, kampuni kama vile Coca- Cola na Adidas zimetishia kujitoa kwa kuwa hazijapendezeshwa na tuhuma hizo, hapo utaona ni kwa kiasi gani umakini unavyohitajika katika kusimamia kazi kama hizo.

Sefue ataka simu kuripoti unyanyasaji


KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ametaka kuwepo kwa namba maalumu ya simu (hotline) itakayotumiwa na makatibu muhtasi kwa ajili ya kupeleka malalamiko dhidi ya unyanyasaji.
Alisema hayo jana mjini hapa wakati akifungua Kongamano la Tano la Kitaifa la Makatibu Muhtasi na Mkutano Mkuu wa Tatu wa Mwaka, unaofanyika mjini hapa chini ya maandalizi ya Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSAE).
Balozi Sefue alisema miongoni mwa mambo yanayomuudhi ni unyanyasaji wa kijinsia ndani ya utumishi wa umma na kutaka kuwe na namba hiyo maalumu, ili yeyote atakayenyanyaswa kijinsia awe na mahali pa kupeleka malalamiko yake ili hatua zichukuliwe.
Kwa upande mwingine alikitaka chama hicho kuendeleza jitihada za kuhamasisha wanachama wake kujiendeleza kielimu, kwa kuwa elimu inapoongezeka na ujuzi umekuwa ukiongezeka pia.
Alisema Makatibu Muhtasi ni watumishi wa kutegemewa kuliko watu wanavyofikiri kwa kuwa wamekuwa kiungo muhimu katika ofisi.
Pia alisisitiza umuhimu wa kutunza siri kwani siri zinapovujishwa madhara yake huwa makubwa huku akiahidi Serikali kuangalia upya viwango vya mishahara kwa watumishi hao.
Alishauri vyuo vikuu kuanzisha shahada maalumu ya taaluma hiyo, ili watumishi hao wajiendeleze kwa ngazi ya shahada na ngazi nyingine.
Awali mlezi wa chama hicho, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Dk Mary Nagu alikitaka chama hicho kuendeleza mpango wa kuanzisha Chama cha Kuweka na Kukopa, ili wajiinue kiuchumi na kufanya kazi kwa bidii katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TAPSEA, Festo Melikio alisema kongamano hilo limehudhuriwa na wanachama 1,005 ambao wamesajiliwa na kuongeza kuwa usajili unaendelea kwa lengo la kupata wanachama 3,000.

Hivi ndio visiwa kumi vyenye mvuto zaidi duniani… Afrika kiko kimoja tu, ni TZ au? (Pichaz)


Hivi ndio visiwa kumi vyenye mvuto zaidi duniani… Afrika kiko kimoja tu, ni TZ au? (Pichaz)madeira
Nimeona nikusogezee pichaz za hivi visiwa 10 ambavyo viko kwenye list ya vinavyoongoza kwa kuwa na mwonekano mzuri zaidi duniani.. Afrika tunawakilishwa na kimoja, unadhani kitakuwa ni cha TZ?
pro
1. Providenciales – Uturuki
maui
2. Maui – Marekani
roatan
3. Roatan – Honduras
santo
4. Santorini – Ugiriki
koh
5. KO TAO – THAILAND
madeira
6. Madeira – Ureno
madeira
bali
7. Bali – Indonesia
mau
8. Mauritius
bora
9. Bora Bora- French Polynesia
nooo
10. Fernando De Noronha- Brazil
©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved