Alichokisema Tox Star Kuhusu Nyimbo Yake Mpya Chillax

Interview Ya Tox Star Alio Ifanya Akiwa Jijini Mbeya Kuhusiana Na Nyimbo Yake Mpya Akiwa Na Barnaba Chillax. Tox Star Alipiga Story Na New Day Taarifa Kuhusu Jinsi Alivo Jupanga Kuhusiana Na Game Jinsi Linavokwenda Saizi.
Pia Tox Star Aliwashukuru Shabiki Zake Kwa Kumpokea Vizuri Pia Na Wadau Kupokea Nyimbo Yake Vizuri.
Vivo Hivyo Video Inaendelea Kufanya Vizuri Katika Channel Mbalimbali Za Hapa Nyumbani Na Nje Pia Kama Trace Na MTV..
Kuangalia Interview Nzima Link Hii Hapa Chini..
https://www.youtube.com/watch?v=vy-iChwhSC4&list=PLlIsYIYscWvZ-SpGaf8GO49mBt9zVYCR9

Tizzy B Afunguka Kuhusu Ngoma Yake Mpya Ya Dear Mchepuko

Leo Hii Tizzy B Afunguka Ndani Ya Media Na Kuachia Ngoma Yake Ya Dear Mchepuko,

Imeachiwa Rasmi Leo Hii Na Inapatakana katika Mitandao Mbalimbali Ya Kijamii..
Ukiachana Na Nyimbo Ya Dear Mchepuko Tizzy B Aweka Wazi Malengo Yake Kuhusu Mausiano Na Mpenzi Wake Kwamba Ni Kwenda Kutoa Posa Ivi Karibuni.
Tizzy B Afunguka Pia Kuhusu Changamoto Katika Maisha Kwamba Ni Kukatishwa Tamaa Na Watu, Ila Kwa Upande Wake Amesema anachukulia Ni Changamoto Tu  Za Kawaida Na Zinazidi Kumuongezea Nguvu Ya Kupigana Kimziki.
Neno La Mwisho Alilo Sema Tizzy B Kwa Mashabiki Ni Kwamba ''Naitaji Support Yenu Ili Tuweze Kufika Sehemu Flani Kwa Kushare Na Kupost pia katika mitandao Yetu Ya Kijamii Ili Tuwezeshe Mziki Wetu Kufika Mbali''..
Kupata Ngoma Hii Gusa Link Hii Apa http://www.mtiwadawa.com/2016/10/download-tizzy-b-dear-mchepuko.html
Kwa Hayo Na Mengine Mengi Kaa Nasi New Day Taarifa.

Walicho Kisema Walio Fika Fainali Kwenye MashindanoYa Fiesta Super Nyota

Wasikilize Ammy Chiba, Zax 4Real Na Selementally Walicho Kisema Baada Ya Mashindano Walipo Kutana Na New Day Taarifa Hapa https://www.youtube.com/channel/UCAe5cIoUh-SGI-mXB1lBluQ

Wadau Mbali Mbali Wa Mziki Watoa Maoni Yao Kuhusu Super Nyota Mbeya

New Day Taarifa Yapiga Story Na Watu Mbalimbali Ambao Ni Wadau Wa Mziki Mbeya Na Kutoa Maoni Yao Kuhusu Mashindano Ya Fiesta Super Nyota Mbeya 2016.
Watu Walio Bahatika Kupia Story Na New Day Taarifa Ni Pamoja Na Robert Elia, Nasir Green, Producer Gachi, Essem Creator, Dj Hiplus, Nolesy, Zax B, Na Wengine Wengi, Ambao wamefunguka kiundani sana ..
Kuwasikiliza Bofya Link Hapa https://www.youtube.com/channel/UCAe5cIoUh-SGI-mXB1lBluQ

Mashindano Ya Fiesta Super Nyota Mbeya 2016

Mashindano Makubwa Ya Kutafuta Vipaji Vya Mziki Fiesta Super Nyota Mbeya 2016 Yamalizika Apo Jana Baada Ya Mshindi Kupatikana Ambae Atawakilisha Mbeya Katika Mashindano Ya Super Nyota Taifa.

Walio Fanikiwa Kupenya Adi Fainali Yani Tatu Bora Ni Zax 4Real, SeleMentally Na Mwanadada Ammy Chiba.
  Na Mwanadada Ammy Chiba Ndie Alie Ibuka Kidedea 
 
Baada Ya Kuongea Na New Day Taarifa, Bi Dada Ammy Chiba Alifunguka Kwa Kusema
''Mi Namshukuru Sana Mungu Kwa Kunisaidia Adi Nimemaliza Mashindano Salama Na Adi Nimeibuka Mshindi Wa Shindano Hili La Leo, Pia Nawaahidi Sito Waangusha Watuwangu Wa Mbeya Nitawawakilisha Vizuri Mbeya''.

Msanii Castor Boy Afunguka Haya Kuhusu Mziki Anaofanya

Castor Boy
Castor Boy Alipo Kutana Na New Day Taarifa Alikua Na Yakusema Kuhusu Mziki Wake Jinsi Anavyo Uendesha Na Kuusimamia..
Castor Boy Alisema,
''Naitwa Castor Boy mwanamziki kutoka nyanda za juu kusini nikiwa nawakilisha vema mkoa wa mbeya nafanya muziki wa aina zote/yoyote japo nimejikita zaidi na Bongo Flavour (R&B) zaidi mahadhi ya zouk. Kimsingi muziki nimeanza kufanya nikiwa na umri Mdogo sana Ila toka nijitambua mi ni nani katika jamii na nafanya nini nikiwa na umri wa miaka 16''..

''Mpaka sasa nmefanikiwa kurecord nyimbo takribani 10 zenye radha tofauti pia nyimbo zangu nmejaribu kufanya studio mbali mbali ili kuleta utofauti wa project iliyopita ya saivi na itayokuja kazi zangu nazisimamia mwenyewe sina msimamzi zaidi nategemea tu namna ile nashirikiana na watu wanaonizunguka''.

Na Tulipo Ongea Na Castor Boy Kuhusu Ngoma Yake Ya I Feel Alifunguka sanaaa na kusema.
      ''Daaah aisee kila ninapokutana na jina hili I feel huwa nashusha kwanza pumzi kwani ni nyimbo iliyotumia muda mwingi hadi kukamilika. I feel ni nyimbo ambayo idea yake niliitengeneza nikiwa na hisia zake kama inavojieleza na kwa upande wa uandaaji beat ulikamilishwa na brother Jeff master Ila kwa upande wa vocal na mixing nmefanya na Emmynelly Bway pale Touchz Music Moro town na ni nyimbo nnayo iheshimu kwa asilimia kubwa coz imenisogeza sehemu flani''.

Na Ukafika wakati wa Kujua Mipango Yake Kiujumla Castor Boy Akasema..
''Mipango yangu kiujumla nikutaka timiza ndoto zangu zaidi kwa kupalilia kipaji changu pia naitaji Fanya mapinduzi kwasababu kuna vitu vilivyopo kwenye Sanaa mbaka sasa naviona havipo sawa so naitaka kuja kivingine..

Kupata Video Ya Castor Boy I Feel Link Hii Hapa //www.youtube.com/watch?v=fBQTF_ywShc
©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved