Msanii Castor Boy Afunguka Haya Kuhusu Mziki Anaofanya

Castor Boy
Castor Boy Alipo Kutana Na New Day Taarifa Alikua Na Yakusema Kuhusu Mziki Wake Jinsi Anavyo Uendesha Na Kuusimamia..
Castor Boy Alisema,
''Naitwa Castor Boy mwanamziki kutoka nyanda za juu kusini nikiwa nawakilisha vema mkoa wa mbeya nafanya muziki wa aina zote/yoyote japo nimejikita zaidi na Bongo Flavour (R&B) zaidi mahadhi ya zouk. Kimsingi muziki nimeanza kufanya nikiwa na umri Mdogo sana Ila toka nijitambua mi ni nani katika jamii na nafanya nini nikiwa na umri wa miaka 16''..

''Mpaka sasa nmefanikiwa kurecord nyimbo takribani 10 zenye radha tofauti pia nyimbo zangu nmejaribu kufanya studio mbali mbali ili kuleta utofauti wa project iliyopita ya saivi na itayokuja kazi zangu nazisimamia mwenyewe sina msimamzi zaidi nategemea tu namna ile nashirikiana na watu wanaonizunguka''.

Na Tulipo Ongea Na Castor Boy Kuhusu Ngoma Yake Ya I Feel Alifunguka sanaaa na kusema.
      ''Daaah aisee kila ninapokutana na jina hili I feel huwa nashusha kwanza pumzi kwani ni nyimbo iliyotumia muda mwingi hadi kukamilika. I feel ni nyimbo ambayo idea yake niliitengeneza nikiwa na hisia zake kama inavojieleza na kwa upande wa uandaaji beat ulikamilishwa na brother Jeff master Ila kwa upande wa vocal na mixing nmefanya na Emmynelly Bway pale Touchz Music Moro town na ni nyimbo nnayo iheshimu kwa asilimia kubwa coz imenisogeza sehemu flani''.

Na Ukafika wakati wa Kujua Mipango Yake Kiujumla Castor Boy Akasema..
''Mipango yangu kiujumla nikutaka timiza ndoto zangu zaidi kwa kupalilia kipaji changu pia naitaji Fanya mapinduzi kwasababu kuna vitu vilivyopo kwenye Sanaa mbaka sasa naviona havipo sawa so naitaka kuja kivingine..

Kupata Video Ya Castor Boy I Feel Link Hii Hapa //www.youtube.com/watch?v=fBQTF_ywShc

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved