Makandarasi waagizwa kujenga barabara bora

http://www.24tanzania.com/wp-content/uploads/2013/01/9159John-Magufuli.jpg
John Magufuli
MAKANDARASI walioko chini ya Wakala wa Taifa wa Barabara (TANROADS) mkoani Kagera wameshauriwa kufanya kazi kwa viwango ili barabara walizokabidhiwa kujenga ziweze kupitika kwa urahisi ikiwa ni njia ya kukuza uchumi wa wananchi wa mkoa huo.
Ushauri huo ulitolewa juzi na aliyekuwa Meneja wa Tanroads mkoani hapa John Kalupale wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika mjini Bukoba.
Mhandishi huyo amehamishiwa mkoani Arusha na nafasi yake imechukuliwa na Andrew Kasamwa kutoka Tanroads Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Kalupale alisema kuwa huu ni wakati wa waandisi hasa chipukizi kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa kama mikataba yao ya kazi inavyoelekeza ili Taifa liweze kupata tija ikiwemo kukuza uchumi wa wananchi kwa kutumia barabara.
“Nawashauri waandisi na kuwaomba fanyeni kazi kwa umakini na kujituma hasa nyie mnaochipukia ili muweze kurithi nafasi zetu sisi pindi tutakapostaafu kazi,” alishauri Kalupale.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo John Mongella, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera alisema ni wajibu wa waandisi kushirikiana na Serikali yao ili kuhakikisha barabara zinatengenezwa kwa viwango na kukamilika kwa wakati kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha.
Wakati huo huo Meneja wa Tanroads mkoani Kagera Mhandishi Andrew Kasamwa aliahidi kushirikiana na wafanyakazi wenzake kwa hali na mali ili kufikia malengo waliojiwekea kikazi.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved