Vijana wajasiriamali wazidi kuwezeshwa na Airtel Fursa

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, imelenga kuwawezesha vijana wajasiriamali wadogo nchini.
Mpango huo wa Airtel umetoa msaada mwingine tena jijini Dar es Salaam kwa msichana mjasiriamali, Bertha Benedicto.
Bertha ambaye amelelewa katika kituo cha kulea watoto cha Dogodogo Center kilichopo Bunju, Dar es Salaam na kuhitimu mafunzo ya mwaka mmoja ya ufundi wa kushona nguo kituoni hapo, amepatiwa vifaa mbalimbali pamoja na cherehani ya kisasa ili kuendeleza ujuzi wake.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi alisema: “Airtel tumeona ni vyema kupitia mpango wetu wa Airtel Fursa kumpatia vifaa na mashine hii ya kisasa ya kushonea Bertha kwa lengo la kumwezesha kuendesha shughuli zake za kiuchumi kwa ufanisi zaidi”.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Bertha amesema vifaa hivyo vitamwezesha kuendesha maisha yake na familia kwa ujumla huku mama yake Immaculate Makinda akiishukuru Airtel kwa kuwa mkombozi kwao.
Naye Mratibu wa Dogodogo Centre, Issa Buzohela alisema, anaiomba kampuni ya simu ya Airtel kuendelea kukisaidia kituo hicho na kuinua vipaji vya vijana kwani nchi yetu imezungukwa na vijana wenye vipaji mbalimbali lakini hawana uwezo wa kuendeleza vipaji vyao.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved