Bob Junior Kuja Na Albam 'Ukweli Wangu', Awashilikisha T.I.D Na Shaa

Muimbaji na mtayarishaji wa muziki Bob junior amesema yuko mbioni kuachia albam yake 'Ukweli Wangu" lakini pia collabo zake na T.I.D pamoja na Shaahttp://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2015/01/Bob-Junior-Sharobaro.jpg Bob junior amesema kuwa baada ya kuona ameshindwa kumpata Jose Chameleone ili washoot video ya wimbo alio mshirikisha, ameamua kujikita kwenye maandalizi ya albam pamoja na kolabo zake mbili.
 "Unajua bado tunapishana na ratiba za Chameleone" amesema muimbaji huyo "sasa nimeamua kuandaa kwanza albam yangu 'ukweli wangu' hii itazungumzia maisha yangu, itakua na nyimbo 8 au 10, ili kabla ya kutoa albam nina kolabo mbili ambazo naanza kushoot video zake wiki ijayo.
Nina kilabo na Shaa ambayo inaitwa 'Bado Bado', pia siku iyoiyo tuna shoot video nyingine ya kolabo mimi na T.I.D inaitwa niguse nayo ni kolabo. kwaiyo mashabiki wakae mkao wa kula kuna mzigo unakuja,.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved