Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba |
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema hayo bungeni jana, alipotoa ufafanuzi kwa Mwongozo kwa Spika ulioombwa na Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM).
Rage katika Mwongozo wake huo, alitaka kusikia kauli ya Serikali kuhusu walimu wapya ambao wamepangwa katika Manispaa ya Tabora na sehemu nyingine nchini kuwa hawajapewa fedha zao na wanaishi katika hali ngumu kwa sasa.
Naibu Waziri alikiri kuwa ni kweli wapo walimu katika baadhi ya halmashauri nchini, hawajalipwa fedha zao baada ya kuripoti kazini kutokana na sababu mbalimbali.
“Ni kweli wapo walimu hawajalipwa fedha zao kama alivyoeleza Mheshimiwa Rage. Yapo maeneo kadhaa nchini na hii imetokana na matatizo kati ya wizara husika na hazina,” alisema Mwigulu na kuongeza: “Ni kama nilivyoeleza hapa juzi kuwa watumishi wanapopangwa ni lazima kila kitu kikamilishwe, sasa hapa kulikuwa na tatizo katika maandalizi yao.
“Lakini jana (juzi) watu wa Hazina wamenihakikishia kuwa shilingi bilioni kumi zimeshapelekwa huko na sasa ni suala tu la kufikishwa kwa wahusika.”
Serikali ilitangaza kuanza kwa ajira za walimu wapya Mei Mosi mwaka huu. Idadi ya walimu wapya walioanza ajira hizo ni 31,056 ambapo kwa walimu wa ngazi ya Cheti ni 11,795, Stashahada 6,596 na wenye Shahada 12,665.
Chanzo Habarileo
No comments:
Post a Comment