RAPA wa muziki wa kizazi kipya, Khery Sameer ‘Mr Blue’, amesema
anamshukuru mzazi mwenzake kwa kumfanya aachane na matumizi ya bangi,
pombe, sigara, mirungi na kuishi maisha ya kawaida.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Blue alisema mpenzi wake aliyemtaja
kwa jina moja la Wahyda, amemfanya aache kutumia vilevi hivyo kutokana
na kumwambia madhara yake.
“Alhamdulillahi nimeamka salama nikiwa mwenye furaha, ahsante
Mungu,na nashukuru pia kwa kufaulu mtihani wa kuacha vilevi asante sana
mke wangu Wahyda,” alisema.
Alisema anamshukuru mpenzi wake kwa kufanikisha kuacha vilevi vyote
bangi, sigara, mirungi, pombe na kuishi kama binadamu wa kawaida.
Alitumia nafasi hiyo, kuwashauri ndugu zake rafiki zake wa karibu
wanaotumia vilevi hivyo kuachana na matumizi ya vitu hivyo kwa ajili ya
kukwepa kuharibiwa maisha yao.
mungu amsaidie..
ReplyDelete