Ligi Kuu Bara kuanza Agosti 22

Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto
LIGI Kuu Tanzania Bara, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22, mwaka huu huku dirisha la usajili kwa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu wa 2015/2016, limefunguliwa rasmi jana.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto alisema kuanzia jana dirisha la usajili limefunguliwa hadi Agosti 6, mwaka huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au kusitishiwa mikataba ni kuanzia Juni 15 hadi 30, mwaka huu.
Alisema kipindi cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15, mwaka huu hadi Julai 30, mwaka huu ikiwa ni pamoja na kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya Agosti 7 hadi 14, mwaka huu.
Kuthibitisha usajili hatua ya awali ni Agosti 15 hadi 19, mwaka huu.
Alisema usajili hatua ya pili utaanza kati ya Agosti 17 na Septemba 8, mwaka huu, ikiwa ni pamoja kupitia na kutangaza majina ya pingamizi hatua ya pili ya usajili ni kuanzia Septemba 8 hadi 14, mwaka huu. Uthibitisho wa usajili hatua ya pili ni Septemba 15 na 17, mwaka kuu.
Kizuguto alisema wachezaji wanaotoka nje ya Tanzania, usajili wa mtandao TMS wa Fifa umekuwa wazi kuanzia jana hadi Septemba 6, mwaka huu na klabu zinazosajili wachezaji kutoka nje zinatakiwa kufanya hivyo kupitia akaunti zao za mtandao wa TMS.
Alisema kwa klabu ambazo hazina akaunti ya TMS zinatakiwa kuwasiliana na TFF ili mameneja wao wa usajili wapatiwe mafunzo ya TMS, na baadaye kuombewa akaunti hizo FIFA.
Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL),  inatarajiwa kuanza Septemba 12, mwaka huu, wakati Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajia kuanza Oktoba 17 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved