Multi-millionea na HipHop superstar P Diddy
ameingia kwenye headlines za leo baada ya kujikuta matatani na polisi
kwa kosa la kumshambulia kocha wa mpira katika mazoezi ya mechi ya mpira
ya mwanae katika chuo cha UCLA.
Msanii huyo alikamatwa kwenye majira ya saa sita na nusu mchana kwenye maeneo ya Acosta Athletic Training Complex, na kufunguliwa file la makosa hayo, japo hakuna mtu yoyote aliumia P Diddy
aliweka selo kuanzia saa sita hadi saa kumi na mbili na kuachiliwa
baada ya kushindwa kupata kisa kamili cha kwa nini shambulio hilo
lilitokea.
Lakini licha ya P Diddy kuachiliwa, polisi wamesma milionea huyo alitakiwa kufikishwa jijini Los Angeles kwenye County Sheriff’s Department Inmate Reception Center na bado mipango hio inaendelea.
No comments:
Post a Comment