Wafugaji mkoani Kagera wamuomba KINANA kuingilia kati mgogoro wao



Wafugaji mkoani Kagera wamuomba KINANA kuingilia kati mgogoro wao

Baadhi ya wafugaji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa wamemuomba Katibu Mkuu wa CCM Taifa ABDULRAHMAN KINANA kuingilia kati mgogoro baina yao na idara ya wanyamapori katika mikoa yao ili kujenga uhusiano mwema kati ya pande hizo Mbili.

Wakingumza mara baada ya KINANA kuwasili katika kijiji cha NYAKANAZI wilayani BIHARAMULO mkoani KAGERA, wafugaji hao kutoka mikoa ya KAGERA, GEITA na KIGOMA wamesema kuwa wamekuwa katika mgogoro na idara hiyo ya Wanyamapori na hivyo kuathiri shughuli zao za ufugaji kwa zaidi ya miaka Mitano sasa.

VENANCE MZUKA ni mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya chama cha wafugaji kanda ya ziwa, akadokeza kuwa jitihada kadhaa zimefanyika bila ya mafanikio.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved