Wananchi wakumbushwa kutunza mazingira

Wananchi wakumbushwa kutunza mazingira

Wakazi wa kata ya KINOLE wilayani MOROGORO wamekumbushwa kutunza na kuhifadhi mazingira ili kukabilina na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea kujitokeza katika sehemu mbalimbali nchini.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira Dunia ambapo mtandao wa vikundi vya wakulima nchini –MVIWATA umeamua kuadhimisha siku hii katika soko la wakulima lililopo katika kata ya Kinole tarafa ya mkuyuni wilaya ya Morogoro.

Mtendaji wa kata JOSEPH CHAMDOMA,mwakilishi wa mkurugenzi wa MVIWATA THOMAS LEIZER na katibu tarafa ya mkuyuni GRACE TIMOTH hawakuwa na ujumbe mwingine zaidi ya kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kupanda miti kwa wingi ili kudhibiti ongezeko la joto huku akitoa mfano wa india ambapo zaidi ya watu 1000 wamefariki nchini humo kutokana na ongezeko la joto.

Jumla ya miche 300 imepandwa katika eneo la mradi wa MVIWATA ambapo kauli mbiu ni uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali za asili.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved