Wajasiriamali waomba kuandaliwa mazingira bora

Wajasiriamali waomba kuandaliwa mazingira bora

BAADHI ya vikundi vya wanawake wajasiliamali katika manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa vimeiomba serikali kuandaa mazingira mazuri ya upatikanaji wa vifaa vya kuzalishia mali na masoko ya uhakika ya bidhaa zao ili kuwawezesha kufanya biashara zenye faida katika juhudi zao za kukabiliana na umaskini.

MWENYEKITI wa moja ya vikundi hivyo kiitwacho KITAPANDA women Mary Bukindu amewaeleza wahitimu wa mafunzo ya siku kumi ya jinsi ya kutengeneza keki zenye maumbo mbalimbali kuwa moja ya changamoto zinazovikabili vikundi vya wanawake vya uzalishajimali ni uduni wa vitendea kazi na uhaba wa masoko ya uhakika.

BIBI Bukindu amesema serikali kupita mamlaka zake mbalimbali inapaswa kuvisaidia vikundi vya ujasilimali vya wanawake na vijana ili kuondokana na uchumi tegemeze na kuwa na fursa ya kupanga mipango yao ya kimaendeleo na kiuchumi na kuongeza wigo wa kukabiliana na changamoto zinazokwamisha maendeleo ya kweli nay ale ya haraka.

RISALA ya wahitimu hao kutoka katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Sumbawanga iliyosomwa na Tuli Anyimike muhitimu Mary Kasansa na pia nasaha za Afisa maendeleo ya biashara kutoka shirika la viwanda vidogo SIDO mkoa wa Rukwa Salome Mwaisomola na pia mkurugenzi wa kituo cha mafunzo ya maendeleo ya biashara na kilimo-GCDE- Martin Haule kwa pamoja wanaelezea jinsi mwanamke anavyoweza kujikomboa kiuchumi.

MGENI rasmi mwakilishi kutoka chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo-TCCIA-Janus Bernad Mfaume hakusita kuhimiza wanawake kujitokeza katika kampeni ya kukabiliana na umaskini bila kuwa tegemezi.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved