YANGA YAANZA 'MDOGO-MDOGO' KARUME...

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiUHvBgYlz0o54FzmcbPU7LHwsOiqINijy_tkLErIIdiwRdwK_9Ws5f2yZ9JyZUzCY2FBLfAtI7PNcZFo6rbZ1MyAP9zDZ2v-LmOSCcAh0rVPARvhjN0HeDGVdCzspER0ZucNNwMLXMXh3G/s1600/Kocha.jpg MABINGWA wa Kandanda Tanzania bara, Young Africans asubuhi hii wanaanza mazoezi kujiandaa na ligi kuu soka Tanzania bara pamoja na michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Maarufu kama Kombe la Kagame inayotarajia kuanza kutimua vumbi Julai 11 mwaka huu.
Kocha mkuu wa Yanga aliyerejea nchini usiku wa kuamkia jana, Hans van der Pluijm analazimika kuanza mazoezi mdogo-mdogo na wachezaji wachache kwani wengi wapo timu zao za Taifa.
Pluijm anaanza kuwanoa vijana wake leo uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es salaam na kufikia Juni 16 mwaka huu wachezaji wote watakuwa wameripoti, ingawa Kpah Sherman raia wa Liberia anatua leo nchini.
Wakati huo huo, Yanga inasubiri Baraka za TFF kuhusu idadi ya wachezaji 10 wa Kigeni aliopendekeza wasajiliwe kuelekea msimu ujao, lakini tayari imeeleza kwamba ina majina yote ya wanandinga inaowataka.
“Wachezaji wa Kigeni tumeshawapata, tunachosubiri ni TFF kutangaza idadi tunayoruhusiwa kusajili. Tuliomba idadi iongezwe kutoka watano wa sasa mpaka kufikia 10, wakitoa Baraka zao, basi tutatangaza wachezaji tuliozungumza nao na imebaki kuwasainisha tu”. Amesema katibu mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroha.(VICTOR)

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved