Mkataba wa mchezaji huyo unamalizika mwisho wa msimu na hajapewa mkataba mpya.
Beki
huyo wa umri wa miaka 35, aliyejiunga na klabu hiyo akiwa na umri wa
miaka 14, ameshinda Ligi ya Premia mara nne, Kombe la FA mara tano na
Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara moja akiwa na The Blues.
"Ningependa sana kuendelea kukaa, lakini klabu inaelekea upande tofauti,” amesema.
Terry amechezea Chelsea mara 696 na anatumai kuendelea kucheza, ingawa si katika klabu nyingine Uingereza.
"Walisema kwamba
meneja mpya akija, mambo huenda yakabadilika,” Terry alisema baada ya
klabu hiyo kulaza MK Dons 5-1 katika raundi ya nne Kombe la FA.
“Kwa
sasa sijapata mkataba. Nilitaka kujua sasa kama ilivyokuwa awali kila
Januari na hili huchukua miezi kadha kukamilishwa. Hautakuwa mwisho
nilioutarajia. Sitastaafu soka nikiwa Chelsea, imechukua siku kadha
kukubali hili.”
Baadaye hata hivyo, msemaji wa klabu alisema huenda Terry akapewa mkataba mpya.
"John
ameshauriwa kwamba ingawa kwa sasa hajapewa mkataba wowote, kwamba hali
inaweza kubadilika miezi kadha ijayo,” msemaji wa klabu hiyo alisema
baadaye Jumapili.
“Klabu hii inamheshimu sana John na kuthamini yote ambayo ametusaidia kutimiza kufikia sasa.”
No comments:
Post a Comment