Baraza la vijana wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema
limesema lipo tayari kuona Chadema inachelewa kuingia ikulu kuliko
kupeleka ikulu viongozi wenye nia ya kujinufaisha na rasilimali za nchi
zilizopo huku watanzania walio wengi wakiendelea kuteseka kwa maisha
magumu.
Mwenyekiti wa baraza la vijana wa chama cha Demokrasia na maendeleo
Chadema Patrobus Katambi ameyeyasema hayo wakati akizungumza na mamia ya
wakazi wa mji wa Tarime mkoani Mara ambapo amesema Chadema kamwe haipo
tayari kukimbilia ikulu kujinufaisha badala yake wapo tayari kuchelewa
kuingia ikulu kwa kuwapeleka viongozi waadilifu wenye uchungu na taifa
hili ambapo mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Tarime Lukas Ngoto amesema
Chadema haitasita kufanya maamuzi magumu kwa wanaotaka kukigawa chama
hicho.
Nae mwenyekiti mstaafu wa Bavicha John Heche akizungumza na wananchi wa
tarime baada ya kufanya maandamano makubwa kutoka Silali hadi Tarime
ambapo amesema wakati sasa umefika kwa wananchi wa Tarime kufanya
maamuzi magumu kuwapa ridhaa viongozi wenye uchungu na mateso ya
wananchi wenye utayari wa kupigania rasilimali za Tarime zitumike
kubadilisha maisha ya wananchi na sio kuendelea kunufaisha mikono ya
watu wachache.
No comments:
Post a Comment