Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema
vita dhidi ya mapambano ya kudhibiti matumizi na biashara haramu ya
madawa ya kulevya ni mbaya hivyo serikali inaendelea kuelekeza nguvu
zake bila kuchoka wala kupata kigugumizi kuhakikisha hali isiendelee
kuwa mbaya zaidi na kuitokomeza kabisa.
Rais Kikwete ameyasema hayo mjini Bagamoyo mkoani Pwani baada ya
kupokea maandamano ya wadau wa kupinga matumizi na biashara hiyo
waliobeba mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho ya
kitaifa ya kupinga biashara haramu ya madawa ya kulevya na matumizi yake
yaliyobeba kauli mbiu tujenge jamii maisha na utu wetu bila madawa
inawezekana.
Awali kamanda wa kupambana na kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya nchini kamishna Godfrey Nzowa amesema licha ya
Sheria mpya ya kudhibiti madawa na biashara ya madawa itasaidia
kufanya kazi hiyo kwa ufanisi lakini bado kuna changamoto kadhaa
zinazowakabili ikiwemo ugumu wa kupambana na wasafirishaji wa madawa
hayo maeneo ya baharini.
Katika maadhimisho hayo Rais Kikwete alizindua mtandao wa kusaidia
vijana (TAYOA) kupiga simu bure ili kujua namna ya kujizuia na kujikinga
dhidi ya madawa ya kulevya huku baadhi ya walioathirika na madawa hayo
wakitoa ushuhuda mbele ya Rais Kikwete na kumshukuru kwa jitihada zake
za kuwaokoa ambapo balozi wa kupinga madawa hayo Rehema Chalamila
kupitia taasisi yake ya Ray C ametoa wito kwa jamii na vijana kuachana
na matumizi ya madawa hayo.
No comments:
Post a Comment