Hatimae serikali imeundoa mswada wa
sheria ya upatikanaji habari wa mwaka 2015 bungeni ili kutoa fursa kwa
wadau na kamati ya maendeeo ya jamii kuendelea kuujadili na kutoa maoni
zaidi kwa lengo la kuboresha sheria hiyo.
Akitoa taarifa ya serikali bungeni, waziri wa nchi ofisi ya rais
asiye na wizara maalum, Prof Mark Mwandosya amesema serikali imetafakari
maoni ya kamati na kuafiki mswada uendelee kufanyiwa kazi hadi kamati
ya maendeleo ya jamii itakapokamilisha kazi yake na kuwasilisha maoni
yake bungeni.
Wakati huohuo bunge limepitisha mswada wa sheria ya kuanzisha na
kusimamia vituo vya pamoja mipakani wa mwaka 2015, ambapo akiwasilisha
mswada huo, naibu waziri wa fedha Mhe.Adam Malima amesema lengo la
sheria hiyo ni kuondoa changamoto zilizopo sasa za kukaguliwa mara mbili
au zaidi kwa mizigo kwa ajili ya kukamilisha taratibu za forodha,
ucheleweshwaji wa mizigo na kuvuja kwa mapato.
No comments:
Post a Comment