BLATTER AJIUZULU URAIS FIFA


Rais wa FIFA, Sepp Blatter ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo.
Sepp Blatter akiwapongeza wajumbe wa FIFA baada ya kushinda nafasi hiyo siku sita zilizopita.
Maafisa wakuu wa FIFA waliokamatwa siku mbili kabla ya uchaguzi.
MTIKISIKO, Rais wa FIFA Sepp Blatter (79) ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Urais wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kufuatia kashfa ya rushwa.
Taarifa iliyotolewa leo makao makuu ya FIFA mjini Zurich, Uswisi, Blatter amesema anaondoka baada ya miaka 17 kama mtu mwenye nguvu katika soka.
Blatter ataendelea kubaki madarakani hadi hapo Fifa itakapofanya uchaguzi mkuu mpya wa viongozi na unatarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Blatter alichaguliwa tena wiki iliopita baada ya kumshinda Prince Ali licha ya maafisa wake saba wakuu kukamatwa siku mbili kabla ya uchaguzi.
Blatter alijiunga na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) mwaka 1975 kama mkurugenzi wa kiufundi, akawa katibu mkuu (No.2) mwaka 1981, na baadaye kutawazwa kuwa urais.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved