Producer, Rapper na DJ wa muziki Marekani, Dj Khaled siku chache zilizopita alikuwa kwenye Interview moja ya Radio ndani ya Los Angeles, Marekani.
Kati ya mambo waliyoongelea kuna kitu kimoja nimekijua baada ya kumsikia kwenye Interview hiyo… DJ Khaled aliulizwa kwa nini hapendi kutumia usafiri wa ndege>>>“…aah
bwana mimi ndege zinanipa presha, sio utani, pale ndege inapoanza
kuondoka uwanjani kuna ule muungurumo na mtikisiko wa ndege inapoanza
kupaa… ile mimi inanipa tumbo joto yani hua napanic, natoa jasho
natetemeka na vitu kama hivyo yani!! kibaya zaidi unakuta Pilot wa ndege
anatoa tangazo kua hali ya hewa itakua mbaya safari nzima! Hapo
inamaanisha safari nzima tutakua tumeshikilia roho zetu mkononi!
Inanikera sana yani, natamani wangekua wanasema mapema ili nigeuze
palepale Airport, lakini wajanja hawakuambii!!”
Swali jingine likawa linahusu njia anayoitumia kusafiri safari za mbali, DJ Khaled alisema >>“….mimi
kusafiri natumia basi na nimenunua private bus yangu kurahisisha kazi,
yani hata iwe safari ya wapi nitakuja na basi, hata kuja hapa Los Angeles
kwa ajili ya hii interview nimekuja na basi, hapa nlipo nina miaka 6
ama 7 sijapanda ndege na wala sina mpango wa kubadilisha msimamo huu”.
Kuhusiana na show za Kimataifa je??>>>“nipo
kwenye mpango ambao bado unaendelea wa kununua boti yangu.. yes nipo
kwenye mpango wa kufanya hicho kitu kwa sababu niko serious kabisa
sitaki kupanda ndege… hata kama ikitokea basi itokee tuu ila
asinishawishi mtu kitu chochote kuhusu kupanda ndege…sipendi na
ninaogopa!“
No comments:
Post a Comment