David De Gea kwenda Madrid

https://res.cloudinary.com/the-news-hub/image/upload/v1412677214/yfrxqwg0ghumrszvbgsp.jpgHabari ambazo mashabiki wa Manchester United wamekuwa wakihofia kuzipata hivi karibuni hatimaye zimekuwa kweli baada ya kipa namba moja wa klabu iyo Mhispania David De Gea kuiambia klabu hiyo kuwa anataka kuhamia Real Madrid .  De Gea kupitia wakala wake ameiarifu United kuwa dhamira yake ni kujiunga na Madrid na amefikia uamuzi huo baada ya kipindi kirefu cha kuwaza na kuamua ni hatua ipi bora ya kufuata kwenye mustakabali wake .  De Gea amekaa na United kwa muda wa miaka minne tangu aliposajiliwa toka Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho ambayo iliweka rekodi kwa makipa ya paundi milioni 17 na amekaa United kwa muda wa miaka minne , muda ambao amepia hatua kubwa kiasi cha kufikia kuwa na kiwango cha ubora wa dunia .  Hivi karibuni De Gea alipewa ofa ya kuongezewa mshahara mpaka kufikia paundi 200,000 kwa wiki ofa ambayo hajaikubali akiwa amefikia uamuzi wa kurudi nyumbani kwao kwenye mji aliozaliwa na kukulia huku akipata fursa ya kuwa karibu na mpenzi wake Edurne .  De Gea amekuwa kwenye mipango ya Real Madrid kwa muda mrefu ambapo klabu hiyo imemuweka kama chaguo namba moja la kuziba nafasi ya mkongwe Iker Casillas ambaye umri wake unazidi kuwa mkubwa .  Endapo usajili huu wa David De Gea kuondoka United na kuhamia Hispania kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu , kipa huyo atakuwa mchezaji wa tano kuondoka United baada ya Cristiano Ronaldo , David Beckham , Ruud Van Nistelrooy na Gabriel Heinze. Klabu ya Manchester United ya nchini England imetangazwa kuwa klabu yenye thamani kuliko zote duniani kufuatia utafiti uliondeshwa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita , utafiti uliohusisha klabu kubwa za soka duniani .
Thamani ya United imeongezeka maradufu kutokana na mikataba kadhaa ya udhamini na biashara ambayo imekuwa ikiingia kila mara chini ya uongozi wa Mkurugenzi wa klabu hiyo Ed Woodward .
Chini ya uongozi wake thamani ya United imekuwa kubwa hali ambayo imefanya timu hii kuwa na fedha ambazo zinaipa kiburi cha kuwa na uwezo wa kufanya usajili wa nguvu bila kuhofia minyororo ya kanuni ya financial fair play .
Bayern Munich wanashika nafasi ya pili katika orodha ya klabu zenye thamani kubwa kuliko zote duniani .
Bayern Munich wanashika nafasi ya pili katika orodha ya klabu zenye thamani kubwa kuliko zote duniani .
United inafuatiwa na klabu za Bayern Munich na Real Madrid ambazo zimefuatana katika orodha kwenye nafasi ya pili na ya tatu huku Manchester City na Chelsea zikikamilisha orodha ya 5 bora .
Fc Barcelona ambayo ubingwa wa ulaya iliyoutwaa juzi umeiongezea kipato cha paundi milioni 28 iko kwenye nafasi ya sita nyuma ya Man City .
Sababu kubwa ya kupanda kwa thamani ya Manchester United ni Mkurugenzi wake Ed Woodward ambaye chini ya uongozi wake klabu hii imeingia mikataba mingi yenye thamani kubwa .

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved