Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa nyumbani kwake kwa marehemu Kitendagulo, mjini Bukoba mkoani Kagera.Marehemu Luangisa ni miongoni mwa Waasisi wa Taifa na katika vipindi tofauti tofauti alikuwa mkuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi (Kagera),Mbunge na Meya wa Manispaa ya Bukoba pamoja na nyadhifa nyingine.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada
la maua kwenye kaburi la Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa mapema
jana asubuhi nyumbani kwake kwa Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitia
saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Mh. Samuel
Luangisa nyumbani kwake jana, Kitendagulo, mjini Bukoba mkoani
Kagera.(PICHA NA MICHUZI JR-BUKOBA).Article Source: MO Blog
No comments:
Post a Comment