| WAZIRI wa Mawasiliano na Miundombinu Hamad Masoud Hamad na Naibu wake Issa Haji Ussi |
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imeamua kutengeneza Meli mpya ya Abiria MV Mapinduzi 11 pamoja na mizigo
Nchini Korea ili kuwapatia usafiri wa uhakika wa Baharini kwa Wananchi
wa Visiwa vya Unguja na Pemba.
Hayo yameeleza leo na Naibu wa
Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi huko Baraza la Wawakilishi
linaloendelea Chukwani Nje kidogo wa Mji wa Zanzibar wakati akijibu
suala la Muwakilishi Salim Abdallah Hamadi wa Jimbo la Mtabwe aliyetaka
kujua Meli hiyo inatarajiwa kugharimu kiasi gani.
Amesema mradi wa ujenzi wa Meli ya
Serikali itagharimu jumla ya Dola za Kimarekani USD 30,825,000 ikiwemo
malipo ya Msimamizi wa Ujenzi wa Meli hiyo.
Aidha amefahamisha kuwa jumla ya
USD 37,000 zitatumika katika gharama ya safari ya Viongozi wa Serikali
pamoja na wanasiasa waliopata fursa ya kusafiri Nchini Korea ya kusini .
Hata hivyo ameeleza kuwa safari za
Viongozi hao wa Serikali,Wanasiasa na Watendaji wa Serikali
zimegharamia kupitia Bajeti za Wizara na Taasisi zenye dhamana ya
utekelezaji wa mradi huo.
Vilevile amefahamisha kuwa
kulifanyika vikao vya maendeleo ya mradi (Progress Mittings) ambapo
mambo mbali mbali yanayohusu utekelezaji wa mradi yamejadiliwa na
kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa mradi
kabla ya kuruhusu kazi nyengine za mradi huo kuendelea.
Naibu huyo amesema kwa mujibu wa
ratiba ya ujenzi wa Meli hiyo tukio linalofuata la majaribio la Meli
Baharini linawahusu Mabahari wanaopatiwa mafunzo ya uwendeshaji wa Meli
hiyo na kuileta Nchini.
No comments:
Post a Comment