Sitta: Niliwahi kukataa rushwa ya Sh140 milioni

Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta  amesema anasimama kifua mbele kupambana na rushwa kwa kuwa aliwahi kuikataa rushwa ya Dola 70,000 (sawa na Sh140,000) milioni).
Sitta alisema hayo jana wakati akizungumza na makada wa chama hicho waliojitokeza kumdhamini katika wilaya ya Geita mkoani Geita na kusema kuna baadhi ya watia nia wanaopita wakisema kuwa wakiwa marais watapambana na rushwa wakati ukiwatazama macho yao yanaonyesha ni wala rushwa. Viwango vya kubadili fedha za kigeni, kwa sasa Dola moja ya Marekani sawa na Sh2,000.
“Nilitumwa Canada kutafuta ndege tatu, jioni moja tukiwa Canada tunajiandaa kuondoka, akaja mkurugenzi wa masoko wa kampuni tuliyonunua ndege, akaniambia waziri tuna kautaratibu hapa ukifanikisha ndege zetu zikanunuliwa tunatoa bakshishi ya Dola 70,000 utataka hizi hela tuzipeleke benki gani,” alisema Sitta akimnukuu ofisa huyo wa masoko.
“Watazameni hawa watu... mtu kawa waziri mwaka mmoja leo anataka urais, halafu anasema atapambana na rushwa…utapambana na rushwa wapi wakati hata hujapita kwenye mitego ya rushwa. Watazameni kwa makini, mtawajua tu kwa macho, kwani macho yao yamekaa kijanjajanja kweli,” alisema. Aliendelea, “Kwa kuwa mimi nililelewa vizuri nilijua tu huo ni mtego wa shetani, nikamwambia mkurugenzi nitampa jibu kesho, nikawasiliana na wakubwa zangu kwanza wakakubali ni chukue hiyo pesa ikasomeshe marubani wa ndege.”
Sitta aliwataka wananchi hao kuwatazama kwa makini watangaza nia hao, na kuwauliza iwapo tayari walishawahi kupambanishwa na rushwa.
Lowassa aonya kuhusu viongozi wanafiki
Kigoma. Wakazi wa Kigoma wametakiwa kuwa makini na kauli za baadhi ya viongozi wa Serikali wanaojinadi kwa kusema wanawapenda Watanzania maskini, lakini mioyoni mwao hawana huruma.
Hayo yalisemwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa alipokuwa akitafuta wadhamini
mkoani hapa, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu zenye majina ya wanachama waliojitokeza kumdhamini.
Akiwa katika ofisi ya CCM mkoa, Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Nohoji Kubaji alimkabidhi Lowassa fomu 45 za wana CCM waliomdhamini.
“Wapo viongozi, wanajifanya wanawapenda na kuwajali watu masikini, lakini wao wenyewe unawakuta ni matajiri, hawa jamaa ni waongo sana hawa,” alisema.
Lowassa aliwataka wakazi Kigoma kumuombea ili dua na sala zao ziweze kumsaidia afikie malengo aliyojiwekea. “Nina dhamira ya kuwatumikia, lakini lazima mniombee sana dua na sala ili mambo yangu yaende vizuri hatimaye nishinde kuwa Rais wa Tanzania. Mimi nachukia sana umaskini, kwa hiyo lazima tuwe kama Malaysia ambayo kiongozi wake alipambana kuhakikisha wananchi wanaondokana na umaskini,” alisema.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved