TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI KIJIJI CHA MAGOZA, MKURANGA

 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya akikata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa gharama ya sh. mil 56, katika Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang'anda, Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Kushoto ni Diwani wa Kata hiyo, Karu Karavina na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo (wa pili kulia).
 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto kwake) pamoja na Diwani wa Kata ya Kiparang'anda, Karu Karavina (kushoto) wakifurahi baada kukabidhi mradi wa  kisima cha maji kwa wananchi wa Kijiji cha Magoza, wilayani Mkuranga mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL gharama ya sh. mil. 56.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved