Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza kwenye mkutano maalum uliofanyika Ikulu, jijini Helsinki.
Kulia ni mwenyeji wake Rais wa Finland, Mh. Sauli Niinisto.
Rais
Sauli Niinisto wa Finland amemueleza Rais Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 2
Juni, Ikulu, jijini Helsinki wakati wa Mazungumzo baina ya viongozi
hao.
“Uhusiano
wetu ni wa muda mrefu, ni uhusiano ambao umedumu kwa miaka 50, tumekuwa
na uhusiano ambao umeleta maendeleo ya kiuchumi kwa Tanzania”. Rais
Niinisto amesema, na kuongeza kuwa, “Hii inatupa nafasi ya kutafuta
mbinu mpya za kuleta maendeleo na kukuza ushirikiano huu zaidi”.
Rais
Kikwete aliwasili Helsinki tarehe 1 Juni,2015 kwa ziara ya kikazi ya
siku 3 ambapo pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kumshukuru
Rais Niinisto kwa mwaliko wake ambapo amemuelezea hali ya kisiasa,
kiuchumi na kijamii nchini Tanzania.
Rais
pia amemueleza mwenyeji wake kuhusu uchaguzi mkuu ujao nchini Tanzania
na kuweka bayana kuwa, “Nimekuja kukushukuru pamoja na wananchi wa
Finland kwa ujumla kwa mchango na misaada yenu ya maendeleo kwa Tanzania
tangu nchi yetu ipate uhuru hadi leo na bado uhusiano wetu upo imara”.
Rais
Kikwete amesema na kuomba Finland kuendelea kuisaidia Tanzania katika
jitihada zake za kukuza uchumi na kuletea watu wake maendeleo. Rais
Kikwete pia anatumia ziara hii kuwaaga na kuwashukuru viongozi na
washirika wa Tanzania katika maendeleo, ambao wametoa mchango mkubwa na
msaada kwa serikali na wananchi wa Tanzania katika kipindi chake cha
uongozi.
Rais
Kikwete pia amefanya mazungumzo na Wabunge wa Finland ambao ni viongozi
wa vyama vya siasa nchini humo, wakiongozwa na Spika wao Bi. Maria
Lohela. Bi. Lohela amesema, Rais Kikwete ndiye kiongozi mkubwa wa nje
kutembelea na kufanya mazungumzo na Wabunge hao ambao wameshika nyadhifa
zao mpya kuanzia mwezi Aprili mwaka huu.
Rais
Kikwete amemueleza Spika Lohela kuhusu kuisha kwa muhula wa Bunge la
sasa nchini Tanzania ambapo, Spika Lohela amesema bunge la Finland
linapenda kuendeleza ushirikiano na Bunge la Tanzania na hivyo kutoa
mwaliko kwa wabunge wapya watakaochaguliwa katika uchaguzi wa Oktoba,
mwaka huu.
Rais
Kikwete pamoja na mambo mengine, ametembelea chuo Kikuu cha Aalto
jijini Helsinki ambacho ni chuo cha 3 kwa ukubwa nchini Finland. Chuo
cha Aalto kina utaratibu wa kubadilishana wanafunzi na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Rais
Kikwete anatarajia kumaliza ziara nchini Finland tarehe 3 Juni,2015 kwa
kukutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa sekta mbalimbali
kabla ya kuelekea nchini Sweden kuendelea na ziara yake ya kikazi
kufuatia mwaliko kutoka kwa Waziri Mkuu wa Sweden Bwana Stefan Lofven.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Helsinki – Finland
3 Juni, 2015
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Helsinki – Finland
3 Juni, 2015
(DK)
No comments:
Post a Comment