KILELE CHA MAONESHO YA VIWANDA VIDOGO KANDA YA ZIWA (SIDO) YAFANYIKA MKOANI SHINYANGA

Moto ukiwa unawaka katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako leo Juni 2,2015 ndiyo kilele cha maonesho ya bidhaa za viwandani kanda ya ziwa yaliyoandaliwa na shirika la Viwanda Vidogo nchini SIDO.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ndiye aliyefunga maonesho hayo yaliyodumu kwa siku 5 yakihusisha wajasiriamali 260 kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Kabla ya kufunga maonesho hayo ambayo yamefanyika mkoani Shinyanga,mkuu wa mkoa huo Ally Rufunga alitembelea mabanda mbalimbali.
Mwanafunzi Asha Hamis kutoka chuo cha VETA Shinyanga akipanda kwenye mtambo unaitwa Loader na kuonesha utaalam wake wa kufanya kazi kwa kutumia mtambo huo,baada ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kutembelea banda la chuo cha VETA
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akimpongeza mwanafunzi wa VETA Asha Hamis aliyeendesha Loader na mwenzake Jafari ( katikati) aliyeendesha Greda hapo uwanjani.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved