|
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika Equality for Growth (EfG), JaneMagigita
akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) wakati wa ufunguzi
wa Kongamano hilo Dar es salaam leo. |
|
Ofisa
Programu Dawati la Uangalizi wa Serikali wa Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC), Hussein Sengu (kulia) akitoa mada katika Kongamano la
siku mbili la Wanawake Wafanyabiashara Sokoni Tanzania lililofanyika Dar
es Salaam leo. |
Kongamano hilo lililowahusisha wanawake kutoka mikoa
tisa ya Tanzania Bara limeandaliwa na Shirika la Equality for Growth
(EfG)
Wafanyabiashara
wanawake Masokoni wakiwa kwenye Kongano hilo.*************Na Dotto
MwaibaleMKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (Repoa),
Samwel Wangwe amewataka watanzania kuwawezesha wafanyabiashara wadogo
wadogo hususani wanawake kwani wananafasi kubwa ya kuchangia pato la
Taifa.Akizunguza Dar es Salaam leo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la
kwanza la wanawake wafanyabiashara sokoni Tanzania, Wangwe alisema ni
muhimu kuhakikisha wafanyabiashara hao wanawezeshwa na kuwajali katika
uzalishaji na uendeshaji wa biashara zao.Alisema kwa mujibu wa takwimu
mbalimbali zinaonesha kuwa hali ya kiuchumi duniani katika sekta ya
wafanyabiashara wadogo inaendelea kukua hivyo kutoa changamoto kubwa
katika kuhakikisha inawekewa mazingira mazuri ya kisera."Wafanyabishara
wadogo ni wengi sana hivyo wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa
kutokana na uwepo wa asilimia 43 ya wajasiriamali wanawake Tanzania,"
alisema Wangwe.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, alisema lengo la kongamano
hilo ni kuwakutanisha wanawake wafanyabiashara walio sokoni kutoka
katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa lengo la kuwajengea
mshikamano na kujadili masuala muhimu yanayowahusu katika biashara
zao.Alisema kongamano hilo limehusisha wanawake 200 kutoka katika mikoa
ya Mwanza, Shinyanga, Mtwara, Lindi, Mara, Mbeya, Iringa, Dar es Salaam,
na mkoani Tanga katika Wilaya ya Lushoto huku wakiongozwa na kauli mbiu
isemayo 'Sauti ya Mwanamke Sokoni'.Alisema kauli hiyo inalenga
kumkomboa mwanamke mfanyabiashara kwa kumjengea uwezo kutambua yeye ni
nani na nafasi yake kama raia katika kuendesha shughuli biashara za
shughuli za soko.
No comments:
Post a Comment