DSC06174

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida, Diana Chilolo (wa kwanza kushoto) akipokelewa na kikundi cha uhamasishaji cha Nyota cha Mandewa manispaa ya Singida. Chilolo alifanya ziara ya kikazi katika manispaa ya Singida hivi karibuni na kuwataka wanawake kuondoa woga na kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.

DSC06218

Mbunge wa viti maalum mkoa na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida,  Diana Chilolo,akizungumza na wajumbe wa Baraza la UWT Singida vijijini ambapo aliwataka wahamasishane katika kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao.Kulia ni katibu wa UWT mkoa Anjela Robert na kushoto ni Katibu UWT wilaya ya Singida, Hadija Kissuda.

DSC06182

Baadhi ya wajumbe wa baraza la UWT manispaa ya Singida,wakimsikiliza mbunge wa viti maalimu na Mwenyekiti wa UWT mkoa, Diana Chilolo wakati akizungumza nao kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini Singida. (DK)