RAIS wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameshitakiwa katika Mahakama ya
Afrika Mashariki iliyopo jijini Arusha kutokana na hatua yake inayotajwa
kukiuka Katiba ya nchi hiyo kwa kuwania kipindi cha tatu cha Urais.
Kesi hiyo, ambayo pia inamjumuisha Mwanasheria Mkuu wa Burundi, Tume
ya Kitaifa ya Uchaguzi kwa nchi ya Burundi pamoja na Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mujibu wa taarifa maalum kutoka kwenye
taasisi ya mawakili wa Kanda ya Afrika (PALU) inayosimamia shauri hilo.
Hii sasa inamaanisha kuwa kiongozi huyo wa Burundi atahitajika wakati wowote kwenda Arusha mahakamani, kuhudhuria kesi yake.
Ripoti hiyo iliyoidhinishwa na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha
PALU, Jancelline Amsi, imeeleza kuwa shauri hilo namba RCCB 303 la 2015
dhidi ya Nkurunziza liliwasilishwa katika Mahakama ya Jumuiya na Umoja
wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Uganda,
Burundi na Tanzania chini ya mwamvuli wa taasisi yao ya ‘East African
Civil Society Organizations’ Forum (EACSOF).’
Mashirika hayo yanamtuhumu Rais Nkurunziza kwa kukiuka katiba ya nchi
yake pamoja na kuvunja makubaliano ya Amani ya Arusha katika dhamira
yake ya kugombea urais kwa kipindi cha tatu, hatua ambayo imesababisha
machafuko nchini Burundi yaliyopelekea vifo vya wananchi wapatao 70 huku
wengine zaidi ya 140,000 wakiikimbia nchi yao.
Hatua hiyo inakuja wakati Rais Nkurunziza akiwa amejikita katika
kampeni za urais, hivyo kushindwa kujumuika na wakuu wa nchi za EAC
wanaokutana Dar es Salaam kujaribu kutafuta ufumbuzi wa tatizo la
kisiasa la Burundi.
Msemaji wa Rais Nkurunziza, Gervais Abahiro alieleza kutoka Bujumbura
alisema kuwa bosi wake huyo angewasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Burundi, Alain Aime Nyamit
No comments:
Post a Comment