KIPA
wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Juma Kaseja Juma ni miongoni mwa
watakaoshiriki kozi ya makocha wa makipa nchini itakayofanyika Julai 13
hasi 17 mwaka huu mjini Dar es Salaam.
Kaseja
amewika timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na klabu zote kubwa
nchini Simba na Yanga SC na kwa sasa japo hajatangaza kustaafu soka,
lakini ameanza kupata mafunzo ya ukocha.
Katikati
ya msimu uliopita aliomba mwenyewe kujitoa Yanga SC akidai klabu hiyo
ilishindwa kutekeleza vipengele vya Mkataba baina yao na tangu hapo
amekuwa akifanya mazoezi na timu ya makipa nchini.Kozi
hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), itashirikisha
jumla ya makocha wa makipa 29 wa klabu za Ligi Kuu na timu za taifa na
itafanyika katika ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es
Salaam.
Mbani
na Kaseja, wengine ni Juma Nassor Pondamali, kocha wa makipa wa klabu
bingwa Tanzania Bara, Yanga SC, Rafael Mpangala (Mgambo JKT), Adam
Abdallah Moshi (Simba SC ), Khalid Adam Munnisson (Mwadui FC), Choke
Abeid (Toto African), Mussa Mbaya (Ndanda FC), Idd Abubakar Mwinchumu
(Azam FC), Herry Boimanda Mensady (Tanzania Prisons), Kalama Ben Lwanga
(Stand United) na Patrick Mwangata (Mtibwa Sugar).
Wengine
ni Abdi Said Mgude (Coastal Union), Razack Siwwa (African Sports
Tanga), Josia Steven Kasasi (Mbeya City), Ramadhani Juma (Kagera Sugar
Kagera), Abdallah Said Ngachimwa (JKT Ruvu), John Bosco (Majimaji FC
Ruvuma), Fatuma Omary (Twiga Stars), Juma Kaseja Juma (Huru), Athuman
Mfaume Samata (Ilala) na Peter Manyika John (Taifa Stars).
Hussein
Tade Katadula (African Lyon), Juma Mohamed Bomba (Kinondoni), Mwameja
Mohamed Mwameja (Ilala), Agustino Malindi Mwanga (Kigoma), Mohamed
Abbas Silima (Police SC. Zanzibar), Bakari Ali Kilambo (Kizimbani SC
Zanzibar), Hafidh Muhidin Mcha (Zanzibar Heroes), Elyutery Deodatusy
Mholery (Kinondoni), Salim Waziri (Tanga)..
No comments:
Post a Comment