Majeshi yamuaga Kikwete

AMIRI Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Kikwete amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya jeshi katika sherehe za jeshi hilo ambazo pia zilitumika kumuaga rasmi.
Katika sherehe hizo ambazo zilifanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana, walihudhuria wageni mbalimbali. Ndege za kijeshi zipatazo 25 zilipita angani katika uwanja huo kutoa heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu huyo ambaye anamaliza muda wa uongozi wake baada ya uchaguzi mkuu, mwezi ujao.
Kikosi cha Makomando wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi (JWTZ) kilionesha uhodari na ujasiri mbele ya Rais Kikwete. Majeshi hayo ya Ulinzi na Usalama ambayo ni pamoja na JWTZ, Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi Jeshi la Wanaanga, Wanamaji walitoa burudani ikiwa ni pamoja na nyimbo kutoka makundi ya sanaa.
Kwenye sherehe hizo za kumuaga Rais Kikwete ambaye hakuzungumza zaidi ya kushuhudia burudani, zilizofanyika sambamba na maadhimisho ya kuzaliwa kwa JWTZ, Septemba Mosi, 1964.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved