Walioachiwa
huru ni Justina Mungai, Christina Ntemi, Siamini Kombakono, Janeth
Mahenge, Beatha Massawe, Jacqueline Juma, Philimina Mtagurwa na Amina
Mwinchumu.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Warialwande Lema, aliwaachia huru washitakiwa hao jana,
alipokuwa akisoma hukumu ya kesi hiyo iliyochukua takribani miaka
minane.
“Mahakama
hii imewaona washitakiwa hawana hatia na kuwaachia huru kutokana na
upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasi na
kuacha shaka yoyote,” alisema.
Alisema
wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, upande wa jamhuri ulileta
mashahidi sita na vielelezo kadhaa na baada ya washitakiwa kuonekana
wana kesi ya kujibu walijitetea wenyewe na kuleta vielelezo.
Alisema
ni jukumu la upande wa jamhuri kuthibitisha mashitaka pasi na kuacha
shaka yoyote na kwamba sio jukumu la mshitakiwa kuthibitisha kosa hilo.
Hakimu
huyo alisema wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, upande wa jamhuri
uliwasilisha nakala za vyeti na kwamba ulishindwa kuwasilisha vyeti
halisi kuonesha kipi halali na kipi cha kughushi.
Hakimu
huyo alisema pia baada ya kufunga ushahidi pande zote ziliomba
kuwasilisha hoja za kisheria iwapo zinaona washitakiwa wana hatia ama
la, lakini hadi mahakama inatoa hukumu hakuna upande hata mmoja
uliofanya hivyo.
Alisema
upande wa jamhuri haukuleta shahidi aliyetengeneza vyeti hivyo badala
yake walileta nakala tu za vyeti, hivyo upande wa jamhuri umeshindwa
kuthibitisha mashitaka pasi na kuacha shaka yoyote.
Alisema
upande wa jamhuri kama walikuwa na nia ya kuthibitisha kesi wangemleta
mtaalamu wa maandishi ambaye angethibitisha iwapo vyeti hivyo vilikuwa
vya kughushi ama la badala yake imebaki hisia tu.
Hakimu
huyo alisema mahakama hiyo imesikiliza ushahidi wa kuhisi, kwa upande
wa jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka, hivyo imewaona washitakiwa
hawana hatia na kuwaachia huru.
Kwa
mujibu wa hati ya mashitaka, washitakiwa hao walikuwa wakidaiwa
kughushi vyeti vya kuhitimu kidato cha nne na kutoa hati za uongo kwa
mwajiri wao ambaye ni BoT.
No comments:
Post a Comment