Wanachama wa kundi la vijana wanaofanya kazi za sungu sungu huko
kaskazini mwa Nigeria wanasema kundi la wanamgambo la Boko haram
wamechoma vijiji 6 na kuuwa watu 37 katika shambulizi jipya karibu na
eneo la ngome kubwa ya waasi hao katika msitu wa Sambisa.
Vikosi vya vijana hao wanaoiunga mkono serikali viliwaambia waandishi
wa habari Ijumaa kwamba mashambulizi yalitokea Jumatano usiku.Gazeti la
taifa la Nigeria liliripoti kwamba vijiji vyote katika jimbo la
Borno,vilikuwa Koshifa , Matangle , Buraltuma,Darmanti, Almeri na
Burmari.
Mmoja wa askari sungu sungu hao Ahmed Ajimi aliliambia shirika la AP
kwamba waathirika walikuwa wakulima ambao hivi karibuni walirudi
vijijini kwao baada ya askari wa Nigeria kuwaondoa Boko haram katika
maeneo mapema mwaka jana.
No comments:
Post a Comment