Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, aliondoka nchini Afrika Kusini, Jumatatu, akipuuzia masharti ya mahakama ya Pretoria.
Mahakama hiyo ilimtaka yeye kubaki nchini humo mpaka pale itakapo
amua kama anapaswa kukamatwa kwa uhalifu wa kivita na mashtaka ya mauaji
ya halaiki.
Bwana Bashir, alikuwa amevalia vazi lake la kitamaduni, na kupungia
watu kwa kutumia fimbo yake pale alipowasili mjini Khartoum huku akisema
kwa sauti kubwa “mungu ni mkubwa.”
Bwana Bashir alikuwepo jijini Johannesburg kwa mkutano wa umoja wa
Afrika, lakini mahakama ya uhalifu ya kimataifa ilitoa shauri la
kukamatwa kwake wakati akiwa huko.
No comments:
Post a Comment