Kikwete akemea mauaji ya albino


RAIS Jakaya Kikwete amewasihi Watanzania kuacha kuua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), badala yake wawalinde kwani ni aibu kwa baadhi ya watu kuwaua au kushiriki kuwaua wenzao kwa nia ya kujipatia fedha.
Rais Kikwete pia ametoa rai kwa viongozi wa dini kuhakikisha wanakemea mauaji ya albino pamoja na ukataji wa viungo vyao, ikiwa ni pamoja na kufichua wale wanaAlisema Tanzania ina watu wenye ulemavu mbalimbali milioni 2.6 sawa na asilimia 5.8 ya Watanzania wote na kati yao 16,447 sawa na asilimia 0.04 ni wale wenye matatizo ya albino.
Katika kupambana na wimbi la mauaji ya watu hao, Rais Kikwete alisema tangu mwaka 2006/15 watu 139 walikamatwa huku 35 kati yao wakifishwa mahakamani.
Kati ya hao waliofikishwa mahakamani, 25 mashauri yao yanaendelea kusikilizwa, 15 wamepatikana na hatia na 13 wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa, huku wawili wakipewa adhabu mbalimbali na 73 wameachiwa kwa sababu mbalimbali.
Kuhusu madai kuwa Serikali haijachukua hatua kwa watu waliofanya mauaji hayo kwa kuwanyonga, Rais Kikwete alisema kazi ya Serikali ni kukamata na Mahakama inayotoa hukumu ni mhimili mwingine.
Pia aliongeza kuwa kesi za namna hiyo, zinachukua muda kutokana na matakwa ya kisheria, ambapo ni lazima hatua zifuatwe ili kufikia watu kunyongwa. Hata hivyo, alisema Jaji Mkuu, Chande Othman Chande, alimhakikishia kuwa kesi hizo zinatazamwa kwa upekee na zinachukuliwa hatua stahiki.
“Hivi najiuliza kwanini muwaue wenzenu kwa imani potofu? Kila mtu afanye kazi lakini si kuua albino na naomba viongozi wa dini kuwafichua watu hawa maana yawezekana katika nyumba za ibada nao pia wapo, wafichueni na kukemea mauaji haya yanatia doa nchi yetu,” alisema.
Pia alitoa rai kwa halmashauri zote nchini kutumia Bima ya Afya kwa wazee na watu wenye mahitaji maalumu kama wenye ualbino, ili iwe rahisi kupata huduma za afya na kuondoa urasimu usio wa lazima kwa ambao wanahitaji huduma hospitalini.
Alitoa mfano wa wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, ambayo imeanza kutoa matibabu kwa wazee na makundi maalumu ya watu wenye mahitaji kupitia Bima ya Afya, hivyo ni vyema na wengine nao waige mfano huo ili kusaidia upatikanaji wa huduma za afya.
Mwakilishi wa albino hao, Dk Abdallah Possi, ambaye ni mlemavu wa ngozi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), aliomba elimu zaidi ya saratani ya ngozi kwa watu wenye ulemavu huo itolewe kwa umma, na kuondoa urasimu wa upatikanaji wa huduma kwao ofanya mambo hayo kwani baadhi yao ni wachangiaji wazuri makanisani na misikitini, lakini kumbe wanashiriki katika mauaji ya watu hao.
Kikwete alisema hayo jana jijini hapa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi (albino) ambapo alisisitiza kuwa ni aibu na fedheha kwa Watanzania kuua albino.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved