MBOWE AMLILIA MUFTI SIMBA



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za msiba wa Mufti Mkuu wa Tanzania Tanzania, Sheikh Issa Shaaban bin Simba, Kiongozi Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kilichotokea asubuhi ya leo kwa maradhi ya sukari na shinikizo la moyo.

Akitoa salaam za pole na rambirambi kwa waumini wa madhehebu ya Kiislamu na Watanzania wote kwa ujumla baada ya kupata taarifa za msiba huo, Mwenyekiti wa CHADEMA (T), Freeman Mbowe amesema kuwa Mufti Mkuu Simba atakumbukwa kwa namna aliyosimama kama kiongozi wa dini kupitia kauli zake mara kwa mara akisisitiza ushirikiano ndani ya jamii ya Watanzania bila kujali tofauti zao katika itikadi za dini.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved