SERIKALI imewasilisha bungeni miswada sita mipya ambayo imesomwa jana kwa mara ya kwanza.
Aidha, miswada saba inatarajia kujadiliwa na kupitishwa na Bunge
katika hatua zake zote katika vikao vitakavyoanza Juni 29 hadi Julai 8
mwaka huu.
Miswada iliyosomwa kwa mara ya kwanza jana ni ule Muswada wa Sheria
ya Benki ya Posta Tanzania kwa mwaka 2015 iliyolenga kufuta sheria
iliyosajili benki hiyo ili sasa isajiliwe chini ya Sheria ya Makampuni.
Mwingine ni Muswada wa Sheria ya Vituo vya Pamoja Mipakani wa 2015,
Muswada wa Sheria Uwazi na Uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji
Tanzania wa mwaka 2015.
Pia umo Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato na Mafuta ya Gesi wa mwaka 2015 na Muswada wa Sheria ya Petroli wa mwaka 2015.
Kwa mujibu ratiba iliyotolewa kwenye mtandano wa Bunge, miswada
itakayojadiliwa na kupitishwa ndani ya siku 10 kuanzia Juni 29 ni wa
Sheria ya Kupata Habari wa mwaka 2015, Muswada ya Sheria ya Tume ya
Walimu, Muswada wa Sheria ya Kufuta Benki ya Posta, Muswada wa Sheria ya
Kituo cha Pamoja Mipakani.
Mingine ni Muswada wa Sheria ya Petroli na Gesi, Muswada wa Sheria
Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uchimbaji Tanzania na Muswada wa
Sheria ya Usimamizi wa Mapato na Mafuta ya Gesi na Muswada wa Sheria ya
Petroli ya mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment