Trice Beatrice Star wa Mbeya Movie aja na ubunifu wa Tv Show

Trice Beatrice


Msanii anayefanya vizuri kwa upande wa filamu kutoka Mbeya ajulikanaye kama Beatrice"Trice" Kaizaly amekuja na ubunifu wa kuwa na kipindi cha televisheni kinacho kwenda kwa jina la The Whats Up Show.Akielezea kuhusu suala hiloTrice amesema,"Kipindi hiki kinaanza kusambazwa kwanza kwenye mitandao ya kijamii kama whatsapp,facebook na Youtube ili kiwafikie wakazi wengi wa Mbeya na sehemu kabla ya kuchukua hatua za zaidi."
Trice alisema kuwa kipindi hicho kinakuwa kinafanya mahojiano na watu mashuhuri ndani ya mkoa wa Mbeya kwa mfano wasanii,wafanyabiashara,watangazaji na wanamichezo.
Pia alisema kwa sasa wanaendelea kupokea wadhamini kwani wana uhakika wa kukifikisha kipindi kwa watu wengi katika mitandao ya kijamii.
"Ndani kipindi hicho kutakuwa na utoaji wa zawadi na mengi zaidi mbali ya Tatu bora za nyimbo,vipindi vya redio na filam kutoka Mbeya",aliongezea Trice.
Ili watu wakipate kipindi kwa mtandano watatakiwa kwenda Youtube na kutafuta 'Channel' ya New Day Pro Media,au ukarasa wa Facebook wa New Day Pro Media.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved