Director Creator Pro5 Avunja ukimya kutokea Dar

Director Mgisha

Wengi walikuwa wanamfahamu kama moja ya Ma'director' kutoka Mashada Inc Video Production,lakini baadaye akaamia Dar es Salaam ambako nafanya kazi hadi sasa.Baada ya kuifikia NDT Newsroom Creator Pro5  akasema kuwabado anaendelea na tasnia ya videos.
Mgisha aliiambia NDT kuwa "Nimehamia Dar ili kuji'expose' zaidi na kufanya kazi za kimataifa na sio kimkoa".
Baada ya Hapo NDT ikamuuliza kama bado anafanya kazi Mashada au ndio kaamia Dar moja kwa moja,alijibu "Mashada ni studio yangu mama mpaka leo nipo Mashada na tunafanya kazi pamoja".
Baada ya mazungumzo ya hapa na pale ikabidi NDT ipate kujua kiundani juu ya yeye kufanya kazi na kampuni ya Dreams Multimedia ya huko huko Dar kama ni mkataba au inakuwaje?,Creator Pro5 alisema" Sizungumzi kuwa nina mkataba or not but nafanya kazi kwenye kampuni ya Dreams Multmedia Studio na jamaa yangu Robbie Robin."
 Swali la mwisho kwa Creator Pro5  ilikuwa ni kama ameamia Dar moja kwa moja au atarudi Mbeya kuendelea na Kazi?
"Dar siyo moja kwa moja nina 'dream' ya kuwa 'director' bora toka Mbeya na malengo yangu wanambeya wajue wanamuwakilishi mzuri kwenye tasnia ya video na nitaendelea kufanya kazi mbeya"aliongeza Creator Pro5.
Kwa upande wa mafanikio aliyoyapata tangu ameenda Dar Creator Pro5  alisem,"hatua niliyopiga mpaka sasa ni kuongeza skills za video za kisasa na kuongeza marafiki wa muhimu i mean Bongo Music Stars"alimalizia Creator Pro5 .
Tazama Video mpya aliyoifanya Na Chris Robby HAPA .

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved