Walimu washauri kuanzishwa kwa mtaala wa afya ya uzazi

BAADHI ya walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani Rukwa wameelezea umuhimu wa serikali kuanzisha mtaala wa mafunzo ya afya ya uzazi na ujinsia kwa ajili ya wanafunzi wote nchini ili kuwezesha kuelewa fursa sawa kwa mwanamke na mwanaume katika kushiriki uboreshaji wa afya ya jamii na shughuli za kimaendeleo na kiuchumi

WALIMU hao kutoka katika halmashauri za wilaya za NKASI KALAMBO na SUMBAWANGA wameiambia TBC kwa nyakati tofauti wakati wa maandalizi ya kuukabidhi mradi wa mpango wa Afya ya uzazi na ujinsia-TMEP-kwa serikali ya mkoa wa Rukwa, kuwa tofauti kubwa ya kupata haki za kimsingi kati ya mwanamke na mwanaume inachangia kuzorota kwa shughuli za maendeleo

WAMESEMA kutolewa kwa elimu hiyo kwa wanafunzi wote nchini tofauti na ilivyokuwa sasa kwa mikoa miwili ya mradi ya Rukwa na Singida kutawawezesha wanafunzi hao kuepukana na mimba za utotoni sambamba na kuelewa majukukumu sawa kwa mwanamke na mwanaume kwa ajili ya ustawi bora wa jamii

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved