'Watetezi wa haki za binadamu DRC waachiwe huru'

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwaachiwa huru wanachama wao wanaoshikiliwa katika korokoro za nchi hiyo.
Jumuiya 14 za kimataifa na asasi 220 za Kikongo zilitoa taarifa jana zikisisitiza juu ya ulazima wa kuachiwa huru wanaharakati wa haki za binadamu wanaoshikiliwa na vyombo vya usalama vya serikali ya Kinshasa. Fred Bauma na Yves Makwambala ni wanaharakati wawili wa haki za binadamu wanaoshikiliwa kwa miezi mitatu sasa kwa tuhuma za kuchochea machafuko nchini Kongo. Wanaharakati wengine karibu 30 pia wakiwemo Wasenegal na Burkina Faso walikamatwa tarehe 15 Machi katika mkutano wa kubadilishana mawazo juu ya uongozi sahihi barani Afrika. wanaharakati hao wanakabiliwa na tuhuma za kuvuruga nidhamu.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikisumbuliwa na machafuko ya kisiasa katika miezi ya hivi karibuni. Vilevile juhudi zinazofanywa na Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo za kutaka kubakia madarakani baada ya kumalizika muhula wake zimeitia wasiwasi jamii ya kimataifa na kusababisha hali tete nchini humo.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved