AU yaafiki kutuma wataalamu wa kijeshi Burundi

Viongozi wa nchi za Afrika wameidhinisha suala la kutuma wataalamu wa masuala ya kijeshi nchini Burundi.
Katika kikao chao kilichomalizika jana huko Johannesburg nchini Afrika Kusini, viongozi wa nchi za Afrika walichukua uamuzi wa kutuma wataalamu 50 wa masuala ya kijeshi nchini Burundi kwa lengo la kuchunguza mwenendo wa kuyapokonya silaha makundi ya waasi nchini humo.
Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Smail Chergui, amesema kuwa mbali na kusimamia hali ya mambo nchini Burundi, wataalamu hao pia watatoa ushauri kwa polisi ya nchi hiyo iwapo italazimu.
Watu karibu 40 wameuawa na wengine zaidi ya laki moja kukimbia nchi kutokana na machafuko na maandamano yanayoendelea huko Burundi  kupinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa kutaka kugombea muhula wa tatu.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved