Vilio simanzi na majozi vimetawala
katika viunga wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
pale jopo la majaji watatu walipothibitisha pasipo na shaka kuwa Bw
Basil Mramba na Bw Daniel Yona waliokuwa ni mawaziri wa serikali ya
awamu ya pili wanapaswa kwenda jela kwa miaka mitatu na kulipa faini ya
shilingi milioni tano kwa makosa yanaowakabili yakiwemo ya matumizi
mabaya ya madaraka na kuisasabisha serikali hasara.
Katika mahakama hiyo ndugu wawashtakiwa hao walionekana kutoyaamini
yale yanayotokea na wengine kujikuta wakitiririkwa na machozi ambapo
wakati hao wakiwa katika hali hiyo ndugu wa upande wa aliyekuwa katibu
mkuu wizara ya fedha Bw.Gray Mgonja ambaye na yeye alikuwa ni miongoni
mwa washtakiwa walijikuta wanapigwa na butwaa baada ya ndugu yao
kuachiwa huru na mahakama hiyo baada ya kutokutwa na hatia yoyote.
Bw.Mgonja ambaye muda mwingi alionekna kusimama tuu bila ya
kuzungumza chochote alijikuta anaishia na maneno ya kukiambia kituo hiki
pale alipotakiwa kusema lolote zaidi ya kusema hayo yote amemwachia
mungu na yamefanyika kwa rehema za mungu.
Awali wakili wa serikali Tumaniel Kweka amesema Bw Mramba amekutwa
na makosa kumi na moja isipokuwa yona ambaye makosa yake ni pungufu ya
hapa na kwamba watapaswa kulipa fidia ya shilingi milioni tano kwa kosa
la kumi na moja na kama watashindwa kulipa watapaswa kwenda jela kwa
mika mitatu ingwa bado watapaswa kwenda jela miaka mitatu kwa makosa
hayo mengine.
Kwa upande wakili wa utetezi wamesema hawajaridhiswa na hukumu hiyo
na hivyo watakata rufaa ndani ya kipindi kifupi kijacho itakumbukwa
kuwa washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa kuwa walikuwa
watumishi wa umma ambao Oktoba 30 mwaka 2003 walikaidi ushahuri wa
mamlaka ya mapato Tanzania wa kuwataka wasitoe msamaha kwa kodi kwa
kampuni ya Alex Sterwart hatua ambayo iliisababishia serikali hasara ya
mabilioni ya fedha.
No comments:
Post a Comment