JOSHUA NASSARI APATA AJALI YA CHOPA JIMBONI KWAKE..


Mbunge wa Jimbo la Arumeri Mashariki, Joshua Nassari amepata ajali ya Helkopta aliyokuwa akiitumia kufanya ziara jimboni kwake hii leo.

Habari kutoka Arum,eru zinasema kuwa Helkopta hiyo ilipoteza mwelekeo na kwenda kugonga mti na kunasa juu ya mti huo.

Aidha taarifa hizo zinaeleza kuwa Mbunge huyo kwa Tiketi ya Chadema, na rubani wake walitoka wakiwa wazima na wapo katika Hospitali ya Kanila la Kilutheri ya Selian ya jijini Arusha. 

Father Kidevu Blog inatoa pole kwa Mbunge huyo na Wapigakura wake wa jimbo la Arumeru Mashariki kufuatia ajali hiyo na tutawaletea taarifa kamili hapo baadae.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved